Wanusurika kifo basi likipinduka mkoani Simiyu

Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, William Mkonda

Dar es Salaam. Abiria waliokuwa wakisafiri na  basi la kampuni ya Kimotco kutoka Arusha kwenda Musoma mkoani Mara wamenusurika kifo baada ya basi hilo kuacha njia na kupinduka.

Ajali hiyo imetokea leo Alhamisi Septemba 5, 2019 kati ya Itilima na Maswa mkoani Simiyu.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, William Mkonda amesema ajali hiyo imetokea leo saa 12 jioni.

"Hakuna vifo kuna majeruhi ambao bado hawajafahamika na wanapatiwa matibabu katika hospitali ya Maswa. Tunasubiri taarifa ya madaktari wa Maswa ili tutoe taarifa kwa umma,” amesema Kamanda huyo.