Breaking News

Watatu wafa ajalini Mbeya

Tuesday December 3 2019

 

By Yonathan Kossam, Mwananchi [email protected]

Mbeya. Watu watatu wamekufa katika ajali wilayani Rungwe mkoani Mbeya baada ya lori la mafuta kupata hitilafu ya mfumo wa breki na kugonga gari jingine.

Taarifa ya polisi iliyotolewa leo Jumanne Desemba 3, 2019 inaeleza kuwa ajali hiyo imetokea leo saa 4 asubuhi eneo la Kanyegele kijiji cha Ibula kata ya Kiwira.

"Gari aina ya Howo iliyokuwa na tela mali ya kampuni ya Camel Oil ya Dar es Salaam likiwa linatokea Mbeya kwenda Malawi lilipata hitilafu ya mfumo wake wa breki na kugonga gari jingine aina na Canter mali ya Rungwe Spring Water na kusababisha vifo vya watu watatu,” amesema.

Amesema waliokufa ni Frank Samwel Sagumo aliyekuwa dereva wa lori hilo la mafuta, utingo wake aliyetambulika kwa jina moja la Silas na Nelson Samson (35) dereva wa Canter.

Amebainisha kuwa miili imehifadhiwa Hospitali ya Wilaya Makandana.

Advertisement