Waziri Lukuvi atua Arusha kutangaza fidia ya kikongwe aliyedhulumiwa ardhi

Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo  ya Makazi, William Lukuvi 

Muktasari:

Kaya 109 ambazo zipo katika eneo la ekari nane ambalo kikongwe Nasi Muruo (98) amerejeshewa baada ya Rais John Magufuli wa Tanzania kuingilia kati.


Arusha. Waziri wa ardhi Nyumba na maendeleo  ya Makazi, William Lukuvi amefika eneo la Sinoni kutangaza tathimini ya fidia ambayo atalipwa Nasi Muruo (98) mkazi wa eneo la Sinoni, katika jiji la Arusha, baada ya kurejeshwa ardhi yake aliyokuwa anaidai kwa miaka 42.

Waziri Lukuvi ameandamana na mkuu wa wilaya ya Arusha, Gabriel Daqaro na maofisa ardhi na watendaji wengine wa Serikali.

Kikongwe huyu alirejeshewa ardhi yake, Julai 8, 2019 na Waziri Lukuvi, kutokana na maelekezo ya Rais wa Tanzania, John Magufuli, alipomtaka kushughulikia mgogoro huo, hasa baada ya kuripotiwa malalamiko ya Kikongwe huyo, kunayanyang’anywa  ardhi yake tangu mwaka 1977 na ndugu wa ukoo wao, Edward Lenjeshi 

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Agosti 28, 2019, Nasi Muruo amesema anatarajia kujua hatma ya mgogoro huo, hasa baada ya kukamilika upimaji wa ardhi katika kaya 209 zinazoishi katika eneo la ekari nane alilonyang'anywa.

 

"Naishukuru sana Serikali, tumeambiwa Waziri leo anakuja tena kutangaza fidia ambayo nitalipwa baada ya tathimini ikikamilika mimi nasubiri tu," amesema

Wakizungumza katika uwanja wa Sokoni, baadhi ya wamiliki wa viwanja ambao watatakiwa kulipa fidia walisema wanamsubiri Waziri Lukuvi

"Hatupingani na Serikali, natumaimi tutapa haki sawa kwani sisi wengi tuliuziwa tu viwanja na kujenga miaka zaidi 20 iliyopita," amssema Ally Swedi.

Muruo  kwa miaka 42 amekuwa akihangaika kudai, haki yake na licha ya kushinda kesi na kutakiwa kurejeshewa ardhi yake, Mei 22 mwaka 1979 katika baraza la usuluhishi la ardhi  jijini Dar es Salaam n baadaye mahakama kuu.

Hata hivyo, kila ambapo mahakama ilitaka kutekeleza hukumu hiyo, mlalamikiwa Edward Lanjeshi ambaye alifariki mwaka 2018 alikuwa akiweka zuio huku ardhi yake ikiendelea kuuzwa.

Imeandaliwa Mussa Juma,Husna issa na Zainabu Hassan

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa habari zaidi