Waziri Mkuu Sudan aapishwa

Muktasari:

  • Ni Abdalla Hamdok ambaye atashirikiana na Baraza huru kuongoza Serikali ya mpito katika kipindi cha miaka mitatu.

Khartoum, Sudan. Baraza huru la mpito nchini Sudan limemteua Abdalla Hamdok kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo na kuapishwa rasmi.

Waziri Mkuu Hamdok aliapishwa leo Alhamis Agosti 22 katika mji mkuu wa Kartoum siku chache baada ya Baraza hilo kutangazwa rasmi.

Kabla ya uteuzi huo Hamdok alikuwa anafanya kazi katika Umoja wa Mataifa (UN).  Waziri mkuu huyo pamoja na Serikali yake ya mpito inatarajiwa kuongoza Taifa hilo mpaka kipindi cha uchaguzi.

Sudan imemteua Waziri Mkuu mpya ikiwa nchi hiyo ikiwa kwenye utawala wa mpito wa miaka mitatu unaoshirikisha jeshila nchi hiyo na raia. Jumla ya wajumbe kumi na moja wameteuliwa kuongoza Baraza hilo na kuongozwa Luteni Abdel Fattah Abdelrahman Burhan.

Akizungumza mara baada ya kuapishwa, Waziri Mkuu Hamdok alisema kuwa kipaumbele chake ni upatikanaji wa amani na kutatua changamoto ya kiuchumi.