Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Bajeti yagusa huduma zinazotolewa Basata

Muktasari:

  • Bajeti ya Serikali mwaka 2025/26, imetoa mapendekezo ya ada mpya kwa huduma zinazotolewa na Baraza la Sanaa la taifa BASATA, huku DJs, MCs, na wapambaji  wakiguswa.       

Bajeti ya Serikali mwaka 2025/26, imetoa mapendekezo ya ada mpya kwa huduma zinazotolewa na Baraza la Sanaa la taifa BASATA, huku DJs, MCs, na wapambaji  wakiguswa.

Akiwasilisha bungeni bajeti ya mwaka 2025/2026 leo Juni 12, 2025, Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba, amesema Serikali  imetangaza kuwekeza kiwango cha kifedha na sera katika sekta za michezo, burudani na utamaduni kupitia bajeti hiyo ikiwa na lengo la kuchochea ukuaji wa  uchumi, ushirikishwaji wa kijami, na ajira kwa vijana.

Katika kuonesha dhamira ya kweli ya Serikali, bajeti ya Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo imeongezwa maradufu kutoka Sh 285.3 bilioni mwaka 2024/25 hadi Sh519.6 bilioni kwa mwaka 2025/26. Ongezeko ambalo litakuwa muhimu katika sekta hiyo kwenye maendeleo ya taifa.

Serikali imepunguza na kuongeza ada za kujisajili kwenye huduma zinazotolewa na Basata ambapo zitalipwa kwa mara moja, mameneja wa wasanii, producers, wapambaji katika sherehe/matukio, wapiga picha, Mcs, wapambaji wa keki, wapambaji (stylists), miundombinu ya saluni za kike na kiume wote wakitakiwa kulipa 10,000.

Aidha promota wa kazi za sanaa, kampuni zinazotumia wasanii kujitangaza, vyama vya sanaa, wasanii binafsi kutoka nje wanaoishi Tanzania, lebo za muziki, studio za muziki, wakilipa 50,000. Huku Djs akijisajili kwa 40,000.

Hata hivyo, kwa ada za mwaka kwenye upande wa kupata vibali wasanii binafsi watalipa 200,000, wasanii binafsi wa nje ya nchi wanaoishi nchini kwa vibali halali watalipa 50,000, Lebo ya Muziki (Music label 100,000) na Studio za kurekodi muziki zikilipa 50,000.

Kwa upande wa meneja wa wasanii kibali watalipia 50,000, Djs 40,000, Mcs, 100,000, huku producer ikiwa ni 50,000. Hata hivyo, kwa kampuni za ndani za usambazaji wa muziki katika majukwaa ya kidigitali kutozwa 500,000, na kampuni za kigeni za kusambaza muziki zikitozwa Sh2 milioni.