Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diddy apunguziwa kifungo

Muktasari:

  • Page Six, inaeleza  kwa mujibu wa taarifa kutoka gereza la ‘Federal Bureau of Prisons’ tarehe ya kuachiliwa kwa Diddy imebadilishwa kutoka Juni 4, 2028 hadi Aprili 25, 2028. 

Marekani. Rapa na mtayarishaji maarufu wa muziki kutoka Marekani, Sean "Diddy" Combs, amepunguziwa kifungo cha mwezi mmoja na nusu,baada ya kukubali kuhudhulia katika matibabu ya waraibu wa dawa za kulevya.

Page Six, inaeleza  kwa mujibu wa taarifa kutoka gereza la ‘Federal Bureau of Prisons’ tarehe ya kuachiliwa kwa Diddy imebadilishwa kutoka Juni 4, 2028 hadi Aprili 25, 2028. 

Hatua hiyo ya kupunguziwa muda inakuja baada ya Diddy kukubali kujiunga na matibabu ya urekebishaji wa waraibu wa dawa za kulevya (Residential Drug Abuse Program – RDAP) tangu Novemba 2025. Kupitia taarifa hiyo msemaji wa Diddy ameeleza msanii huyo amechukulia kwa uzito mchakato huo huku akionyesha dhamira madhubuti ya kutaka kubadilika.

Hii sio mara ya kwanza kwa tarehe ya kuachiliwa kwake kubadilishwa. Novemba 2025, muda wa kifungo uliongezwa kutoka Mei 8, 2028 hadi Juni 4, 2028 baada ya madai ya ukiukwaji wa kanuni za gereza.

Utakumbuka Diddy amewahi kuhusishwa katika ukiukwaji wa kanuni za gereza. Ikiwemo kutengeneza pombe ya kienyeji akiwa gerezani pamoja na kukutwa na simu, jambo ambalo ni marufuku gerezani.

Kwa upande wa Diddy alidai hakufahamu kuwa simu za aina hiyo haziruhusiwi. Huku msemaji wake akisisitiza simu hiyo ilikuwa inalindwa kisheria chini ya faragha ya mawasiliano kati ya wakili na mteja. 

Wakati kifungo chake kikizidi kupunguzwa muda zaidi, Diddy ameendelea kutaka kuachiwa huru. Ambapo mwishoni mwa Desemba 2025 aliwasilisha rufaa kupinga hukumu yake akiomba aachiwe huru au adhabu yake ipunguzwe. 

Kupitia nyaraka hizo alizowasilisha mahakamani, anadai waendesha mashtaka walishindwa kuthibitisha kesi dhidi yake. Na kwamba hukumu iliyotolewa ilikiuka haki zake za kikatiba. Hata hivyo Februari 2026, waendesha mashtaka waliwasilisha majibu yao wakipinga ombi hilo.

Diddy amekuwa gerezani tangu alipokamatwa Septemba 2024. Alikabiliwa na mashtaka ya kula njama za uhalifu wa kupangwa (racketeering conspiracy), biashara ya ngono kwa kutumia nguvu, udanganyifu na vitisho, pamoja na kusafirisha watu kwa lengo la kujihusisha na ukahaba.

Baada ya kesi iliyodumu kwa miezi miwili, mahakama ilimkuta na hatia katika makosa mawili ya kusafirisha watu kwa lengo la kujihusisha na ukahaba, huku ikimuondolea mashtaka mengine. Kwa sasa anatumikia kifungo katika gereza la Shirikisho  ‘Fort Dix Federal Correctional Institution’