Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diddy msanii aliyetafutwa zaidi Google 2024

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa TechCrunch, jina la Diddy limetafutwa zaidi duniani kote hii ni kutokana na kukabiliwa na tuhuma za unyanyasaji wa kingono, usafirishaji haramu wa watu huku kesi yake ikianza kusikilizwa Mei 5, 2025.

Marekani. Mkali wa Hip-hop kutoka Marekani, Diddy Combs ambaye amezuiliwa katika Gereza la MDC Brooklyn lililopo jijini New York, ametajwa kuwa msanii aliyetafutwa zaidi kwa mwaka 2024 kwenye mtandao wa Google.

Kwa mujibu wa TechCrunch, jina la Diddy limetafutwa zaidi duniani kote hii ni kutokana na kukabiliwa na tuhuma za unyanyasaji wa kingono, usafirishaji haramu wa watu huku kesi yake ikianza kusikilizwa Mei 5, 2025.

                        

Diddy alikamatwa Septemba 16, 2024 katika moja ya hoteli iliyopo jijini New York, ambapo kabla ya kukamatwa nyumba zake zilipigwa msako na kukutwa mafuta zaidi ya chupa 1000.

Katika orodha hiyo iliyoongozwa na Diddy, namba mbili imeshikwa na Usher, Linkin Park, Sabrina Carpenter, Justin Timberlake, Angela Aguilar, Drake Bell, Tracy Chapman, Dave Grohl, huku namba kumi akiwa Angelina Mango.

Utakumbuka aliyekuwa akiongoza kutafutwa katika mtandao huo kwa mwaka 2023 ni Cristiano Ronaldo, nyota wa soka anayecheza Klabu ya Al Nassr kutoka Saudi Arabia na Timu ya Taifa ya Ureno.

Hiyo ilitokana na kufanya kwake makubwa katika soka hadi kupelekea kushinda Tuzo ya Maradona kutoka Globe Soccer kama Mfungaji Bora kwa mwaka 2023 akiwa na magoli 54.