Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hata Volodymyr Zelenskyy alianza kama Shilole, Baba Levo, Mkojani

Muktasari:

  • Ikabidi nikumbuke majina ya wote ninaowadai ile nazama kwenye simu kutafuta majina ya wadeni wangu ili niwavutie waya. Nikakutana na jina la bishoo mmoja wakujiita Zelenskyy. Jina alilojipa mwenyewe akiamini siku moja atakuwa Rais kama Volodymyr Zelenskyy kiongozi wa Ukraine.

Dar es Salaam. Jana mida flan hivi, mdogo mdogo wakati narudi nyumbani nikiwa natoka zangu Jangwani kupiga kelele na kina Mzize. Nikakumbuka mfukoni sina hata mia, mawazo yakahama kutoka Jangwani hadi kwenye kelele za wapangaji wenzangu nisipotoa hela ya umeme usiku ule.

Ikabidi nikumbuke majina ya wote ninaowadai ile nazama kwenye simu kutafuta majina ya wadeni wangu ili niwavutie waya. Nikakutana na jina la bishoo mmoja wakujiita Zelenskyy. Jina alilojipa mwenyewe akiamini siku moja atakuwa Rais kama Volodymyr Zelenskyy kiongozi wa Ukraine.

Lile jina likanipumbaza kidogo kwanza kulisoma ilikuwa tabu, nikajikuta nafananisha harakati za Zelenskyy kutoka kwenye usanii hadi kuwa Rais na za mastaa wa Bongo ambao mwaka huu wanaonekana kujitosa kwenye siasa huku baadhi yao wakitia nia kugombea viti mbalimbali nchini.

Nikaendelea kumuwaza Zelenskyy ambaye kabla ya kuwa Rais alikuwa mchekeshaji wa kikundi la Kvartal 95. Huku akiingiza sauti katika filamu za katuni kama Paddington Bear.
 

Nikakumbuka pia alikuwa akiigiza kama "Rais wa Ukraine" katika kipindi cha TV kilichoitwa "Servant of the People" (2015–2019). Na hatimaye akawa Rais kweli. 

Ile narudisha akili kwa wadeni wangu ikanijia picha ya mwigizaji Arnold Schwarzenegger ambaye licha ya usanii wake aliingia kwenye siasa na kuwa Gavana wa California (2003–2011).

Nikajikuta nasahau shida zangu nikamkumbuka Charles 'Jaguar' Kanyi ambaye ni msanii wa muziki lakini naye alijiunga kwenye siasa na kuwa Mbunge wa Starehe (2017–2022). John Kiarie 'KJ', mwigizaji maarufu wa kipindi cha "Redykulass kutoka Kenya ambaye ni Mbunge wa Dagoretti South na wengine kibao wanaoishi kwenye harakati hizo za siasa.

Hilo nikaliona pia hapa nchini ambapo kwa mwaka huu 2025 wasanii zaidi ya saba wamejitosa kutia nia kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu unaofanyika mwaka huu.


Baba Levo

Clayton Revocatus 'Baba Levo' ambaye ni mwanamuziki na mtangazaji nchini ametia nia na kuchukua fomu kugombea jimbo la Kigoma Mjini kupitia CCM. Utakumbuka Baba Levo amewahi kuwa Diwani wa Mwanga Kaskazini (ACT-Wazalendo) Manispaa ya Kigoma Ujiji.


Mkojani

Mwigizaji Abdallah Mohamed Nzunda (Mkojani) naye ni miongoni wa wasanii walioamua kujitosa kuchukua fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Temeke.



Shilole

Msanii Zena Mohamed 'Shilole' ameamua kujitosa kwa kuchukua fomu ya kugombea ubunge wa viti maalumu mkoa wa Tabora.

Katika ukurasa wake wa Instagram Shilole aliandika, "Namshukuru Mwenyezi Mungu mapema leo nimefanikiwa kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa na chama changu cha CCM kugombea nafasi ya Ubunge wa Viti Maalumu mkoa wa Tabora kupitia UWT,"


Kobisi 

Lumole Matovolwa 'Kobisi' mwigizaji ambaye wengi wanafurahishwa na uigizaji wake katika tamthilia ya 'Kombolela' amechukua fomu ya kugombea ubunge Kibaha vijijini.


Madevu

Stanley Msungu, mwigizaji wa Jua Kali amechukua fomu ya kugombea ubunge Kilolo. Huku wasanii wengine ni Mwijaku (Mvomero Morogoro), Mkuwe Abdul 'Mamibaby'( Tabora katika nafasi ya Ubunge Viti Maalum). Naye Dj  Romy Jons ambaye ni kaka wa msanii Diamond amechukua fomu kugombea ubunge Mbagala.

Mbali na hao wanaogombea ubunge yupo Shetta ambaye amechukua fomu ya kugomea udiwani Kata ya Mchikichini Ilala.
Hata hivyo, hii imenikumbusha kuwa haitakuwa mara ya kwanza kwa wasanii Bongo kuingia kwenye siasa na kuwakilisha wananchi Bungeni kwani tayari wasanii kama Joseph Mbilinyi 'Sugu' Mbeya Mjini (CHADEMA). Professor Jay 'Joseph Haule' Mbunge wa Mikumi (2015–2020) CHADEMA.

Hamisi Shabani 'Babu Tale' Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki, Khadija Taya maarufu Keysha Mbunge wa Viti Maalumu kundi la watu wenye ulemavu, na hata marehemu Kapteni John Komba aliyekuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi alifanya hivyo.