Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hazichuji, hazipoi, haziboi

Muktasari:

  • Hilo ni kutokana na jumbe zake zinakuwa na umuhimu kwa tukio fulani kwa wakati huo, nyimbo hizo zimekuwa zikitumika katika matukio ya kisiasa, majanga, misiba, kutoa elimu kwa jamii n.k.

Dar es Salaam.Katika Bongofleva kuna nyimbo ambazo huwa hazipitwi na wakati, kuna nyakati fulani lazima zinarejea kwenye ubora wake na kuwa na maana zaidi, kitu kinachofanya kupingwa sana hasa kwenye vyombo vya habari.
Hilo ni kutokana na jumbe zake zinakuwa na umuhimu kwa tukio fulani kwa wakati huo, nyimbo hizo zimekuwa zikitumika katika matukio ya kisiasa, majanga, misiba, kutoa elimu kwa jamii n.k.
Kwa leo tunakuletea hizi chache ambazo zimetungwa na wanamuziki kama Ferooz, Madee, Nakaaya Sumari, Banana Zorro na Professor Jay, mwanachama wa zamani wa kundi la Hard Blasters Crew (HBC).


Starehe (Ferooz) - UKIMWI
Tukio lolote la kuwakutanisha vijana kuwapa elimu kuhusu virusi vya UKIMWI, ni vigumu ukakosekana wimbo wa Ferooz, Sterehe ambao kamshirikisha Professor Jay. Na ni vigumu kuukosa katika mahadhimisho ya siku ya UKIMWI.


Starehe ni wimbo uliofanikiwa kutoa elimu kwa kiwango cha hali ya juu kuhusu ugonjwa huo huku ukitokea kupendwa na wengi.
Kutokana na mafanikio yake, Ferooz amekuwa akieleza anastahili kupewa ubalozi wa kupambana na UKIMWI maana wimbo wake huo umekuwa ukitumiwa kila wakati katika mapambano hayo.
Wimbo huu ulichangia sana mauzo ya albamu yake ya kwanza, Safari (2005) inayotajwa kuuza nakala (kanda) 200,000 katika wiki yake ya kwanza sokoni. Inakadiriwa kuwa mauzo ya albamu yote Ferooz alipokea zaidi ya Sh150 milioni.


Kazi Yake Mola (Madee) - Misiba
Wimbo wa Madee ‘Kazi Yake Mola’ aliutunga kufuatia kifo cha kaka yake na Babu Tale, Ally Zungu, ni msiba uliomgusa sana Madee kutokana Ally alikuwa na mchango mkubwa katika kundi la Tip Top Connection.


Hata hivyo, wimbo huu kwa miaka mingi sasa umekuwa ukitumiwa sana kwenye misiba ambayo inaligusa Taifa, vyombo vya habari vimekuwa vikiucheza sana katika kipindi hicho kigumu.
Pindi vinapotokea vifo hasa vya watu maarufu na wenye nguvu ya ushawishi hasa katika tasnia ya burudani na michezo, basi lazima wimbo huo uchezwe mara kwa mara.
Ikumbukwe wimbo huo aliyowashirikisha Domo Kaya na Mandojo, ndio uliobeba jina la albamu ya kwanza ya Madee, albamu hiyo ilifanya vizuri sokoni na ndio iliyompatia fedha za kununua kiwanja chake cha kwanza kwa Sh500,000.


Mr. Politician (Nakaaya) - Uchaguzi Mkuu
Katika kila kipindi cha uchaguzi mkuu nchini ni lazima wimbo huu urejee kwenye ubora wake, unakuwa ni kama ndio umetoka, umaarufu wake ni kutokana na maudhui yake kuhusu wanasiasa wanavyorejea kwa wananchi kuomba kura.


Kupitia wimbo huo, Nakaaya Sumari anawakumbushia baadhi ya wanasiasa kuhusu ahadi zao za uchaguzi uliopita ambazo hawajazitekeleza, na bado wanahitaji tena kura zao, ajabu!.
Mr. Politician ni wimbo pendwa kwa wapiga kura ila sio mzuri sana masikioni mwa manasiasa wababaishaji ambao ni wazuri kwenye kutoa ahadi ila hawapo tayari kutekeleza.
Nakaaya alimshirisha M1 of Dead Prezzz, huku Dunga ndani ya 41 Records akisimama kama Prodyuza, ni wimbo uliompatia umaarufu Nakaaya ambaye naye kuna kipindi alijiingiza katika siasa lakini baada ya muda akaachana na mpango huo.
.  


Mama Yangu (Banana Zorro) - Siku ya Mama
Wanamuziki wengi Bongo wameimba nyimbo za kuwatukuza kina Mama, lakini huu wa Banana Zorro ‘Mama Yangu’ umejitengenezea himaya kwenye nyoyo za watu wengi kwa miaka mingi.


Iwe ni siku ya Mama dunia, siku ya wanawake au tukio lolote linalowakutanisha kina Mama, basi wimbo huu kuna asimilia 90 za kusikika na umekuwa ukitumiwa sana na vyombo vya habari kwenye matukio hayo.
Baada ya kushinda mashindano ya Pop Idol upande wa Tanzania mwaka 2001, Banana Zorro akaja kukutana na Miikka Mwamba, mtayarishaji muziki ambaye ndiye alitengeneza wimbo wake huo, Mama Yangu (2003).
Nyimbo nyingine Bongo zilizojizolea sifa hiyo miaka ya hivi karibuni ni ‘Nani Kama Mama’ wa Christian Bella na Ommy Dimpoz, ‘Mama’ wa Kayumba, ‘Mama’ wa Ben Pol na Goodluck Gozbert n.k.


Ndio Mzee (Professor Jay) - Siasa

Katika wimbo wa Professor Jay ‘Ndio Mzee’ alieleza jinsi baadhi ya wanasiasa ni wazuri kutoa ahadi zenye kuvutia kwa wananchi wao lakini hawazitekelezi kabisa, huku nyingine zikionekana kuwa ni za kilaghai na zisizoweza kutekelezeka.



Wimbo huo kutoka katika albamu ya Machozi Jasho na Damu (2001) akimshirikisha Juma Nature amekuwa ukipigwa sana kipindi cha uchaguzi.