Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jide kutoka Mkapa mpaka Mama Samia

Muktasari:

  • Katikati ya masela. Katikati ya machizi muziki. Katikati ya mfumo dume kweli. Dada akatoboa. Haikuwa kazi rahisi. Ni katika wakati mgumu wa msanii wa kike tena wanaoimba kufanikiwa kuteka watu

Dar es Salaam, Alikuwa ‘atisti’ akawa ‘prizenta’ akawa ‘atisti’. Na sasa ni ‘atisti’ na mjasiriamali. Ni Judith Wambura, Komando, Jide, Mama Some Food, Dada Mkuu. Na mwenye asili ya ‘Kanda Maalumu’. 

Katikati ya masela. Katikati ya machizi muziki. Katikati ya mfumo dume kweli. Dada akatoboa. Haikuwa kazi rahisi. Ni katika wakati mgumu wa msanii wa kike tena wanaoimba kufanikiwa kuteka watu.

Jide akapasua katikati kama radi. Okay alisaidiwa, lakini huwezi kusadia mtu asiyejiweza akaweza. Huwezi kuwekeza sehemu ya hasara. Waliomsaidia walijua wanasaidia sehemu yenye faida. Ndiyo!

Kama unaweza kumsaidia asiyeweza akaweza, wangewasaidia dada zao nao wakaimba. Hakuna mtu wa kupoteza pesa kizembe. Jide aliyekamili kisanii akapita katika mikono salama ya sanaa.

Katika ubora wao Sugu, Pro. Jay na kina Nature. Na Jide alikuwa kwenye ubora wake. Sauti yake ikitumika kupamba vile viitikio vya ngoma za wana na kuipeleka Bongo Fleva katika mioyo ya kike. Jide amehusika sana kuijenga ‘gemu’.

Aliteka soko katika dimbwi la masela wa hip hop. Wakati ule ilikuwa ngumu sana wanamuziki wa kuimba kukusanya mtiti wa mashabiki. Wengi walipenda ngoma za kuchana (hip hop). Jide kapitia njia ngumu sana.

Kwa miaka mingi alipambania soko la muziki wake. Pia alitumia muda mwingi kulilia mapenzi Hii ilifanya pisi nyingi za kimjini zimuelewe kinyama. Kwa sababu aliimba kwa niaba yao na wakamuelewa kirahisi.

Wako wapi kina Stara na wenzao kama Unique Sister, Sister P, Zay B. Achana na Ray C ambaye alikuja kwa msukumo wa uwepo wa Jide. Kuna wakati ilionekana kama Jide anabebwa, lakini muda ukawa jibu sahihi ‘ukatupruvu rong’.

Kwa kusikiliza tungo za Jide. Ilikuwa tiba tosha kwa pisi ziliotendwa kimapenzi. Ngoma zake kama Ndindindi na Mambo Matano za juzi, ni tiba kwa waliotendwa.
Hii ilifanya awe na kijiji chake binafsi cha ‘fansi’ kindakindaki.

Kikazi, kibiashara na kimaisha athari za mapenzi hazina tofauti na athari za dawa za kulevya. Wakati wengi wao maumivu ya mapenzi waliyahamishia ulevini. Jide yeye maumivu ya penzi aliyahamishia kwenye biashara ya muziki.

Hakuna alichobakisha kwenye muziki, ila kuna kitu muziki umebakisha kwa Jide. Heshima! Yes, anastahili heshima kweli. Bahati mbaya Wabongo tulishatoa talaka ya heshima. Hatutoi heshima panapostahili heshima. 

Wanamuziki wengi wa kike na wa kiume wametoweka kwenye muziki. Jide yupo na misukosuko yake. Kakomaa kivyake. Mengine tuache kusubiri wapendwa wetu hawa watangulie ndipo tuangushe mamilioni ya sifa. 

Jide ana akili, ugumu wa penzi la kweli alilokosa akageuza pesa. ‘Stresi’ zake za mapenzi zikatunga msururu wa mkwanja kwenye akaunti yake. Kila kitu ni fursa katika dunia ya sasa, ni suala la kufikiri vizuri tu. 

Mr Nice hakukosea katika maisha yake. Ni makusudi ya Mungu ili kusaidia kina Mondi ambao leo wanakumbuka kuwa kuna mambo ya kuwekeza. Bila mifano ya walioyumba tusingeona mijengo ya masela hawa kila kona.

Uwepo wa Jide ni kusudi la Mungu, ili kina Nandy na Zuchu. Wajue muziki ni maisha kamili, siyo lazima uwe na ajira nzuri kama Mwamvita. Kwamba muziki ni zaidi ya posho za kina Halima pale Bungeni Dodoma. Muziki ni utajiri.

Lady Jaydee ni staa wa muda mrefu sana. Ambaye miaka yote amelilinda jina lake kwa wivu mkubwa. Ameipigania heshima yake kwa hasira nyingi. Katika hili la kulinda heshima yake, huyu dada anabaki katika dunia yake. 

Skendo za kibwege na kiki za kindezi, hazikuwa na nafasi kwake. Alichojua ni kuandaa muziki mzuri na kuwapa raia wake. Kutoka Binti Machozi hadi kuwa mjasiriamali mwenye uwekezaji katika maeneo mengi. Siyo poa! 

Ukiwasaka alioanza nao ‘gemu’. Nina uhakika utawasaka kuanzia leo mpaka Xmass usiwaone. Wapo huko walipo lakini Jide yupo hapa tulipo. Toka katika utawala wa Mkapa, mpaka wa Samia, Jide yupo vile vile.

Siyo wanamuziki wa kike wala wa kiume. Wengi kama siyo gereji ya afya, basi wapo katika karakana zao za ‘laifu’ huko. Pigika bovu na ‘laifu’ la Bongo. Wapo wale wajanja waliokimbilia mambele kubeba boksi. Jide akakaza hapa hapa.

Muziki una mazongwe mengi sana. Na ukiona mtu kadumu kama Jide, usijiulize sana mpe heshima yake. Hakuanzisha bendi ya Machozi kwa kujifurahisha. Na hakuanzisha Nyumbani ‘Lonji’ ili alie bata zake.

Hiyo ni miradi ya kimkakati kwa yeyote mwenye akili timamu. Miradi yake ni picha tosha kwamba ni mwanadada anayejitambua. Alijua anataka nini na anatakiwa kufanya nini. ‘Puti samu rispekti’ kwa Komando. Jiiiiiiiiaaaaa!