Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jiongeze: Marioo mkubwa kuliko Bongo Fleva 

Muktasari:

  • Kila zama na kitabu chake. Kitabu hiki kurasa zake zilikosa urafiki wa kudumu na Bongo Fleva. Yes! Achana na Bongo Movie ambao kuwaongelea unahitaji kitabu kizima. Tuitazame Bongo Fleva, kinadharia utadhani ipo juu sana.

Dar es Salaam. Yes! Tumeshatimiza miaka mitano tangu Samia akalie kiti cha Magogoni. Ana siku chache aachie wengine au aendelee kuishi pale Chamwino. Hili lipo juu ya Watanzania. Kumpa nafasi tena au kumnyima.

Kila zama na kitabu chake. Kitabu hiki kurasa zake zilikosa urafiki wa kudumu na Bongo Fleva. Yes! Achana na Bongo Movie ambao kuwaongelea unahitaji kitabu kizima. Tuitazame Bongo Fleva, kinadharia utadhani ipo juu sana. 

Lakini ukweli ni kwamba wapo wachache wanaoibeba Bongo Fleva. Lakini wengine ni wakubwa zaidi kuliko Bongo Fleva yenyewe. Wanapaa juu wakiiacha Bongo Fleva katika tope na mchangani pale Coco Beach.

Bongo Fleva haipo. Wasanii wanatanuka bila kutegemea ‘aidentiti’ ya Bongo Fleva. Zamani Bongo Fleva ilikuwa juu zaidi ya TID, zaidi ya Mr Nice na TAKEU yake. Ndo maana leo hii msanii anakuwa staa peke yake.

Tusidanganyane. Bongo Fleva imeyumba kwa kiasi kikubwa. Halafu watu ni kama hawajali kabisa. Hata vipindi vilivyokuwa vinatambulika kwa jina la Bongo Fleva havipo tena. Kwa sababu Bongo Fleva yenyewe haipo.

Wasanii waliotakiwa kupeleka kwa madijei Bongo Fleva. Sasa hupeleka amapiano, singeli na madude mengine. Anayepeleka Bongo Fleva redioni, runingani wala mitandaoni hakuna. ‘Testi’ ya Bongo Fleva haipo tena.

Mr Nice pamoja na utawala wake mkubwa Afrika Mashariki na Kati. Lakini hakuwahi kuizima Bongo Fleva, licha ya kutambulisha ule muziki wake kwa jina la Takeu. Leo hutofautishi ladha ya muziki wa staa wa Bongo, Sauzi ama Naijeria. 

Zamani nje ya Tizii neno la Bongo Fleva lilikuwa juu zaidi ya wasanii wetu. Leo ni tofauti, nje ya Bongo wasanii wapo juu bila kueleweka wanafanya muziki wa aina gani. Neno Bongo Fleva limetoweka kama nywele kwenye utosi wa Joji Ambangile.