Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

JIONGEZE: Nyumba ya Nandy na Nenga inavutia kuliko nyimbo zao

Muktasari:

  • Lakini kuna tamu zaidi. Ni ya wanandoa vijana wenye majina makubwa mjini. Nandy na Bilnas. Hao wana jambo lao linatembea katika nyoyo za watu wenye akili mtambuka. Wameleta taharuki isiyo umiza.

Dar es Salaam, Unadhani habari kubwa ni ya Mondi na Mwijaku? Yes! Inawezakana pia ukubwa wake unatokana na Mondi kumjibu ‘Jaku Man’. Kwa sababu Mondi kwake kila kitu huchukua nafasi kubwa kwenye jamii.

Lakini kuna tamu zaidi. Ni ya wanandoa vijana wenye majina makubwa mjini. Nandy na Bilnas. Hao wana jambo lao linatembea katika nyoyo za watu wenye akili mtambuka. Wameleta taharuki isiyo umiza.

Yes! Ukichagua kufuatilia hili la Nenga na Nandy. Ni dhahiri unajiweka katika kundi lenye akili msawazo. Vijana hawa wenye ndoa yao tamu, wametuonesha mjengo wao mpya. Bonge la dude babaake.

                    

Oya! Siyo poa kabisa! Pini la maana sana na bwawa la kuogelea lenye umbo kama la gitaa. Hawajahitaji mdahalo wa kujua kama wana ‘meki mane’ ama vipi. ‘Clipu’ ya ‘cribu’ yao ni mdahalo tosha na wenye kuonyesha pesa wanazo. 

Hili ni darasa tosha bila maneno mengi. Bonge la mjengo lenye mahadhi tofauti na umri wao. Yes! Vijana wanatengeneza pesa. Na hii ndiyo maana halisi ya baraka ya ndoa ama watoto kuja na baraka katika maisha.

Na pia haya ni matunda sahihi ya muziki wa kizazi kipya. Muziki umebadilisha ‘laifu’ ya ‘masista duu na mabrazameni’. Kutoka kuwaza kufunga kaunta za bar mpaka kufunga mtaa kwa mijengo. Hii ndiyo yenyewe.

‘Zatizi wasapu’ wana wa mtobo husema hivyo. Kaka na dada zao waliopigania huu muziki. Waliamini muziki ni pesa na maisha kamili. Majibu ndiyo yanaonekana kupitia maisha ya dogo Nenga na dogo Nandy. 

‘No drama no kiki’, kimya kimya kama Jaymoe na Ngwea. Wanaotesha mijengo tu ya maana kweli kweli. Nyumba yao inavutia kuliko nyimbo zao. Usisahau Nandy na Nenga ni wasomi wazuri tu ila muziki unawapa pepo ya dunia.