Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kajala: Siwezi kurudia maisha ya zamani

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwananchi, Kajala alisema uzoefu alioupata katika maisha pamoja na majukumu mapya aliyonayo sasa vimemfanya kuwa makini zaidi katika maamuzi yake na namna anavyoishi maisha yake ya kila siku.

Dar es Salaam. Msanii wa Bongo Movie, Kajala Masanja amesema kuna mambo aliyokuwa akiyafanya zamani ambayo kwa sasa haoni tena sababu ya kuyaendeleza na hatua alizofikia maishani zimembadilisha kwa kiasi kikubwa.

Akizungumza na Mwananchi, Kajala alisema uzoefu alioupata katika maisha pamoja na majukumu mapya aliyonayo sasa vimemfanya kuwa makini zaidi katika maamuzi yake na namna anavyoishi maisha yake ya kila siku.

Msanii huyo alisema kwa sasa amejifunza kutanguliza amani na utulivu wa maisha yake kuliko mambo mengine, akisisitiza si kila jambo linalostahili kupewa nafasi kama ilivyokuwa zamani.

"Kuna mambo nimeyavuka kabisa, siwezi kuyafanya kwa sasa kwa sababu nimekuwa mtu tofauti na ninayaangalia maisha kwa mtazamo mwingine," alisema Kajala.

Mbali na hilo, Kajala alisema kufufuka kwa uhusiano wake na msanii Harmonize kumempa nafasi ya kujifunza mambo mengi, huku akiamini kila hatua ya maisha huwa na funzo lake kwa mtu anayepitia.


Aidha, staa huyo alisema kupata mjukuu pia kumemfanya ajione yupo katika hatua nyingine ya maisha inayohitaji utulivu, busara na kuwaza zaidi kuhusu familia kuliko ilivyokuwa hapo awali.

Kauli za Kajala zinakuja wakati mashabiki wake wakionyesha kuvutiwa na mabadiliko yanayoonekana katika maisha yake, huku wengi wakiamini uzoefu alioupata katika miaka ya hivi karibuni umemsaidia kujenga mtazamo mpya kuhusu maisha na mahusiano.