Kanye West aweka meno ya Sh2 bilioni

Muktasari:

  • Kanye West ameanza mwaka kwa mbwembwe aweka meno ya bandia yenye thamani ya Sh2.1 bilioni adai ametoa meno yake ya asili kuyaweka hayo yaliyotengenezwa na madini ya Titanium

Kuishi kwingi kuona mengi, ndivyo unavyoweza kusema juu ya Rapa wa Marekani, Kanye West ambaye ameondoa meno yake yote na kuweka ya bandia ambayo yametengenezwa kwa madini ya Titanium yanayotajwa kuwa ni ghali zaidi ya madini ya Diamond

Meno hayo aliyoyaweka mwanamuziki huyo  yanakadiriwa kuwa na thamani ya dola za Marekani 850,000 sawa na Sh2.1 bilioni.

Taarifa zilziochapishwa katika gazeti la Uingereza la Daily Mail, zimeeleza kuwa rapa huyo alishiriki kikamilfu katika kuchagua mtindo wa meno hayo ya bandia anavyotaka yawe kwenye kinywa chake.

Gazeti hilo limeandika kuwa daktari bingwa wa meno, Thomas Connelly ambaye ni mmiliki wa kliniki ya Master Dental Technician ndiye aliyehusika kwenye kubadilisha meno hayo ya Kanye West na kumfanya awe na mwonekano tofauti.

Daktari huyo amekiri kufanya kazi na Kanye katika kufanikisha ubadilishaji huo wa meno akieleza kuwa msanii huyo alikuwa na uchaguzi wa kile alichohitaji kufanya kwenye kinywa chake.

Hii si mara ya kwanza kwa Kanye kushughulika na meno yake, kabla ya kuamua kuyaondoa na kuweka aina hiyo ya madini alishawahi kubandika meno yaliyotengenezwa kwa amdini ya Diamond.