Msanii C-Pwaa afariki dunia

Muktasari:

Enzi za uhai wake C-Pwaa alitamba kupitia kundi la Park Lane na nyimbo zake binafsi kama Action aliyomshirikisha Dully Sykes,  Ngwair (marehemu) na msanii kutoka Jamaica Ms.Triniti zilifanya vizuri

Dar. Msanii wa muziki wa kizazi kipya,   Ilunga Khalifa maarufu C-Pwaa amefariki dunia usiku wa kuamka leo Jumapili Januari 17,  2021.

Kifo cha C-Pwaa ambaye enzi za uhai wake alitamba na kundi la Park Lane kabla ya kuanza kufanya muziki mwenyewe kimetokea katika hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kulazwa takribani siku nne.

Akizungumza na Mwananchi Digital muandaaji wa muziki,  P Funk Majani ambaye alikuwa karibu na msanii huyo amethibitisha kifo cha C-Pwaa.

"Ni kweli amefariki lakini mengine mtayafahamu zaidi kutoka kwenye familia yake," amesema Majani.

Wasanii mbalimbali wameguswa na kifo cha msanii huyo aliyeimba nyimbo za Action,  Mmmh na Pwaa

Kupitia akaunti zao za  instagram,  Shilole, Adili, waandaji wa muziki Marco Chali, J Murder na  wameandika ujumbe wakieleza jinsi wanavyomfahamu na mazuri aliyofanya.