Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mwanamieleka Virgil afariki dunia 

Muktasari:

  • Virgil alijulikana zaidi kati ya mwaka 1980 na 1990, kufuatia umahiri wake katika mchezo huo ambao ulimfanya akubalike na Shirikisho la Mieleka duniani (WWE).

Marekani.Mwanamieleka kutoka Marekani, Michael Jones ‘Virgil’ amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 61, baada ya kusumbuliwa na saratani ya utumbo kwa muda mrefu.

Taarifa ya kifo cha staa huyo imetolewa na refa wa Mieleka Mark Charles, kupitia ukurasa wa X (zamani twitter), ambapo ameeleza kuwa Virgil alifariki akiwa hospitali wakati akiendelea kupatiwa matibabu.

Virgil alijulikana zaidi kati ya mwaka 1980 na 1990, kufuatia umahiri wake katika mchezo huo ambao ulimfanya akubalike na Shirikisho la Mieleka duniani (WWE).

Mwanamieleka huyo mahiri mwaka 2022, alitangaza kusumbuliwa na tatizo la ubongo unaoathiri kumbukumbu na uwezo wa kufikiri pamoja na saratani ya utumbo.