Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ni Amapiano tu na hauna la kufanya

Muktasari:

  • Natembea nikichati. Nimetanua mikono kama Makonda wa Daslama ya Magu. Pia mkono mmoja umechoka kupungia washikaji, pisi kali na washua wasiotaka kuzeeka na kwenda kuishi nje ya mji. 

Dar es Salaam, Wikiendi iliyopita. Nikiwa mitaa ya kujidai Sinza. Nakatiza mtaa huu kwenda wa pili huku nikiwaza, nikatulie kiota gani nami nitazame mechi za ligi mbalimbali? Yes! msimu wa ligi ulianza rasmi maduniani kote. 

Natembea nikichati. Nimetanua mikono kama Makonda wa Daslama ya Magu. Pia mkono mmoja umechoka kupungia washikaji, pisi kali na washua wasiotaka kuzeeka na kwenda kuishi nje ya mji. 

Sinza kuna madingi walinunua viwanja enzi hizo kuna fisi na chui kibao. Bado wapo Sinza, hawataki kwenda Msakuzi wala Mwanagati. Hawataki kupumzika Mapinga wala Madale juu au Kibaha.

Wanapishana tu mitaa na totozi ambazo robo tatu ya mwili upo wazi. Robo ndiyo kuna vitambaa vimezibaziba. Sinza ni rahisi kuona mtu amevaa nusu uchi kuliko mvaa suti. Ni ‘fulu’ wazimu na siyo Sinza tu. Nenda Kinondoni nako.

Yes! ‘Jentromani’ nikazama ‘kijentromani’ na kukutana na wana kama wote. Hakika nilienda sehemu sahihi ya kutazama boli. Nikaagiza kinywaji kile niagizacho nikiwa Mwailubi, Royal Village, Miami kama siyo Pestana.

                       

Ni kinywaji ambacho hunipa ujasiri flani wa kiboya. Najiona kama Dotto Biteko au Kamilius Wambura. Katika hali ambayo hata Steve Nyerere ananifunika. Hiki kinywaji kuna wakati hunipa ujasiri hata wa kupiga simu kwa Spika.

Stori na wana zikaendelea, vinywaji vikitawala eneo lote kama Pacome na Nzengeli. Pisi kali zimemwagika kama zote, zinapitapita tu bila kueleweka na pamba zao nyingi ni jezi za Yanga. Yes! Yanga wameuza sana jezi safari hii.

Wana nilikuta wanaponda Amapiano. Eti inaharibu Bongo Fleva. Wao wanalilia utambulisho wa muziki wao wa kitambo hicho. Nawaelewa kwa sababu ukisoma kilometa za umri karibu wote zimesogea sana.

                      

Ni vijana walisoma sekondari enzi za IGP Omar Mahita. RPC wa Dar ni Tibaigana. Enzi hizo CCM muenezi wao ni Omar Mapuri. Nyakati hizo watuma salamu redioni ni maarufu kuliko wachezaji wa Simba na Yanga.

Hoja zao nilikuwa nazielewa vizuri sana. Mjadala ulikolea nilipoibuka. Waliamini najua mambo ya muziki na ningeweza kuwaweka sawa. Tofauti na walivyotaka. Nikaanza kwa kuwachana namna hii.

Hakuna tena! Hakuna utambulisho wetu tena. Na bahati mbaya wanamuziki siyo wabunge kwamba awamu ijayo wote tuwatose. Ni ama ufuata Amapiano au subiri mauti ya Bongo Fleva. Na huna la kuwafanya.

Utaniambia nini? Nimemlipa S2Kizzy hizo milioni kadhaa. Kaninyongea biti flan hivi la Mpiano. Nimeingiza ‘voko’, limeenda maduniani na ‘pipo’ zina ‘pare’ kila klabu. Kuanzia Daslama, Nairobere mpaka Jozii kwa Madiba.

‘Eloti ofu mane’ nimetumia. Mamilioni kwa video, washiriki hadi wapambaji wa wasanii. We umekaa na kikalamu sijui ‘kimaiki’ studio unaponda Amapiano. Kisha ukimaliza kuponda unasubiri mshahara. 

Achana undezi siku moja moja. Hakuna Mangi anayetaka hasara. Nafanya hiyo Amapiano ili inilipe kwa gharama zangu nilizotumia. Nataka nikajenge mjengo wangu na kumuweka sawa ‘bi mkubwa’. 

Oya! Braza. Muziki asili yake ni zile ‘pipo’ choka mbaya. Wa kishua wanaoimba hujifurahisha tu. Tangu na tangu muziki ni liwazo la wenye shida. ‘Weibaki’ toka Paulo na Sila, waliimba kule gerezani ili watoke.

Mtoto wa kimasikini anapotaka kutoboa kupitia muziki. Hawezi kuelewa ukitaka awe mipaka. Eti sijui misingi ya Bongo Fleva. Ni vigumu kukuelewa, atakuona mchawi unayepaswa kuchukiwa.

Leo Bongo Fleva wa kitambo wanaumia. Kuona muziki wao inatoweka wakiwa hai. Wakiwa bado wananyoa viduku nao. Wanataka muziki wao uleule ubaki vilevile. 

Wanakereka Marioo aki-song kimapiano kila siku. Utamu wa Zeze la TID, ufundi wa Chilla na My Boo, undava wa MB Dog na Latifa. Unyama wa Dully na Salome, umetoweka kama nywele za utosi wa Sallam. Watu humu tu... hawana habari!

Unadhani kuna jipya? Hiki kinachotokea, kilitokea wakati ule. Bongo Fleva ilipitia magumu kuliko hizi kelele za Amapiano. Wanamuziki wale wa kitambo walikerwa na Bongo Fleva kama leo wa kitambo wanavyokerwa na Piano. 

                     

Ulionekana muziki wa kihuni, ulichukiwa na jamii ya watu wazima. Walitaka kuona Prof. Jay akiimba kama Hassan Bichuka. Walitamani Inspekta Haroun akimbizane na gitaa kama Hamza Kalala Komandoo. Ndiyo walichotaka.

“Bongo Fleva ilipigwa vita na wengi hasa madingi.” Huu ni mstari wa Profesa Jay katika moja ya ngoma zake. Leo hii wale waliowachana wazee wetu kina Masoud Masoud. Ambao waliona Bongo Fleva kama usanii tu nao wanawachapa hawa madogo.

Leo hii wanalia na kina Marioo. Wanaona muziki wao unafilimbwa na hawa vijana wa Gen Z. Ile dhambi ya kukerwa na kilio cha wazee wa kipindi kile, inajirudia kwa wazee wa sasa. Ni kuhitimisha kwa neno la: “Malipo ni hapa hapa duniani.” 

‘Madijei walichukiwa kwa kupiga nyimbo za kina Juma Nature zaidi, kuliko za kina Chidumule. Walikerwa sana na midundo ya P Funk, walitaka ile ladha ya gitaa la Mwanyiro iendelee kwa kizazi na kizazi.

Watu walitaka kumsikiliza Lady Jaydee na siyo Amina Ngaluma. Ulikuwa wakati wa Zay B na Sister P. Siyo Patricia Hillary na Mwanahawa Ally. Dunia ilihama toka kwenye gitaa na ‘dramzi’ kwenda kwenye CD. Dunia ya kidijitale iliteka.
Ni wakati wao na huna la kufanya.