Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Oscar Oscar kimuziki amepita njia za hawa!

Muktasari:

  • Oscar ambaye ni mtangazaji wa Wasafi FM, amemshirikisha rapa kutokea kundi la Weusi, Joh Makini katika wimbo huo ambao Baraza la Sanaa Taifa (Basata) limeeleza kuwa unapaswa kuchezwa katika vyombo vya habari kuanzia saa sita usiku.

Dar es Salaam. Mtangazaji Oscar Oscar a.k.a Mzee wa Kaliua ameteka mazungumzo mtandaoni wiki hii baada ya kutoa wimbo wake, Mniombee (2025) ambao ukiachana na ujumbe wake ulioacha gumzo, ameonyesha uwezo mkubwa wa kuchana.

Oscar ambaye ni mtangazaji wa Wasafi FM, amemshirikisha rapa kutokea kundi la Weusi, Joh Makini katika wimbo huo ambao Baraza la Sanaa Taifa (Basata) limeeleza kuwa unapaswa kuchezwa katika vyombo vya habari kuanzia saa sita usiku.

Hata hivyo, huyo sio mtangazaji wa kwanza kufanya muziki hasa katika mtindo wa Hip Hop, kuna wenzake wengi walishafanya hivyo miaka ya nyuma hivyo Oscar Oscar amepita tu njia za hawa wafuatao.


Sam Misago

Amefanya vipindi vikubwa vya burudani kama Power Jams (sasa Planet Bongo) cha East Afrika Radio na FNL cha EATV, Sam aliingia kwenye muziki wakati yupo kwenye kile cha mafanikio ya kazi yake ambayo sasa ameipa kisogo.

Sam Misago alifanya muziki kwa kipindi kifupi sana kwa kuachia nyimbo zake kama ‘Nimepania’  akimshirikisha Ben Pol, ‘Vyura na Madanga’ akiwa na Quick Rocka, pia kuna ‘Ballin and Chillin’ akimpa shavu Ude Ude.


DJ Fetty

Hakuna asiyejua mchango wa DJ Fetty katika kuikuza Bongofleva kupitia vipindi kama XXL na Bongo Fleva, pia amehusika kuwatoa wasanii kama Godzilla na Nikki Mbishi kupitia mashindano ya Free Style Emcee Shujaa 2008.

Fetty ambaye sasa anatangaza kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM ni mzuri kwenye kurap, alisikika kwenye wimbo ‘Chizika Remix’ wa kundi la Fly But Ghetto (F.B.G) pamoja na G Nako, pia amechana kwenye ngoma ‘Shangwe’ iliyotoka kwa ajili ya Fiesta.

Dullah Planet

Mtangazaji huyu wa Crown FM ni mpenzi sana wa muziki wa Hip Hop na kwenye vipindi vyake vya redio amekuwa akiupa nafasi sana pamoja na aina nyingine za muziki Bongo tangu akiwa East Africa Radio na TV kabla ya kujiunga na Crown FM.

Hapo Oktoba 2021 ndipo Dullah Planet aliachia ngoma yake kwanza ‘Unaendeleaje’ akimshirikisha Brown Punch, amerap vizuri na kujielezea yeye ni nani amefanya nini katika muziki wa Bongofleva na kwanini anajiita Rais wa Bongofleva.


Diva

Wakati yupo Clouds FM, Diva aliingia kwenye muziki kwa kishindo kwa kuachia wimbo wake ‘Piga Simu’ akimshirikisha Ommy Dimpoz, kisha ikafuata remix yake ambayo Diamond Platnumz alipewa nafasi.

Diva anayetangaza Wasafi FM kwa sasa alifanya kazi hadi na Mwana FA ila tayari ameupa kisogo muziki na aliwahi kusema anafanya muziki kama sehemu ya kujifurahisha tu wala sio kitu anachokipa muda wake sana maana ana aibu sana.


Adam Mchomvu

Ndiye mtangazaji Bongo aliyetoa nyimbo nyingi zaidi, alitoka kama msanii na wimbo wake, Joniii. Mchomvu alishirikishwa na kundi la Nako 2 Nako Soldiers katika remix ya wimbo wao ‘Mchizi Wangu’, pia ndiye aliyeratibu mpango wa kufanyika remix hiyo.

Mchomvu aliyekuwa anatangaza kipindi cha XXL, na sasa JahaziHD, Clouds FM, ameshirikisha wasanii wengi katika nyimbo zake, miongoni mwao ni Carol Kinasha, TID, JCB, Rosa Ree, Q Chief, Khadija Kopa, Dark Master.