Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tofauti ya Mondi na Alikiba

Muktasari:

  • Ni wakati ambao Mondi gari lake lilishawaka. Akishindanishwa na Rich Mavoko, Belle 9 na Barnaba. Wote aliwakalisha vibaya sana na akawa anaelekea kwenye kilele cha ufalme.

Dar es Salaam, Alikiba. Ndiyo! kuna ‘taimu’ ni kama alisusia flani hivi ‘gemu’ la muziki. Baada ya kuachia Usiniseme na Dushelele. Ukimya wake ukawa ni mkubwa ingawa siyo kwa kipindi kirefu.

Ni wakati ambao Mondi gari lake lilishawaka. Akishindanishwa na Rich Mavoko, Belle 9 na Barnaba. Wote aliwakalisha vibaya sana na akawa anaelekea kwenye kilele cha ufalme.

2010 na 2012 ukiachana na 20%, ni Mondi aliyekuwa pale juu. Ghafla tu Kiba akahojiwa na Sporah Show. Na kauli yake ya “Kiti cha Ufalme, nafuta vumbi nakaa mwenyewe.” Iliamsha hisia za wengi.

Ni kama Wabongo walisubiri mtu wa aina hii ajitokeze aseme kitu chochote ili wamshindanishe na Mondi. Kumbuka wakati huo Mondi kateka kila kitu nchi hii. Muziki wa Bongo unamzunguka yeye.

Usipomuona gazetini, ni runingani au redioni akihojiwa. Akawa ni yeye tu. Hiki kitu Wabongo hawakipendi. Wanachukia kuona mtu mmoja tu anakuwa juu peke yake. Lazima watafute mshindani.

Mondi yule alijua kutengeneza pini za maana. Kujiuza huku akichagiza na uwepo wa pisi kali kama Wema kando yake. Akawa bidhaa yenye mvuto zaidi kuisoma, kuisikiliza na kuitazama. Alikuwa kwenye kilele cha ustaa.

Wabongo wakaona kama Kiba ndio kiboko ya Mondi. Wakatembea na yeye na mashabiki kugawanyika. Na ‘utimu’ ukaanza. Hata ile ngoma ya Mwana, aliyotoa kwa ujio mpya.  ukweli haikuwa tishio kwa Mondi, ilikuwa ya kawaida.

Tayari Mondi alikuwa na utajiri wa pini kali zenye ujazo. Lakini Kiba akabebwa na ile dhana ya kutaka mtu mmoja asiwe yeye tu. Walitaka Mondi apate mpinzani wa kweli kwenye muziki na asijitawale.

Wimbo wa Mwana haukufikia hata ubora wa Nenda Kamwambie wa Mondi. Licha ya kuifanya video yake ‘Sauzi’ bado haikuwa kiviile. Na hata alichomaanisha kwenye mashairi yake kwa walio wengi hawakuelewa.

Diamond alikuwa na njaa kali sana ya kutoboa. Mtu aliyetaka ‘kubato’ naye alipaswa kujipanga sana. Mtu aliyeingia kinyonge angekalishwa dakika sifuri. Alikuwa na njaa ya pesa na umaarufu.

Kiba anatoa Mwana mbele ya Mawazo, Moyo Wangu, Mbagala, Nitarejea. Mbele ya Nataka Kulewa, Ukilala Lala Salama, Ukimuona na Nenda Kamwambie. Dogo alikuwa na hazina ya mipini ambayo mpaka leo bado ni mali.

Wimbo wa Kiba, ulioleta ‘bato’ la kweli kweli ni Seduce Me. Hili goma angetoa kabla ya Mwana, huenda leo tungekuwa tunaongea tofauti. Kabla ya Seduce Me Kiba alikuwa anatoa pini za kawaida zisizo na ushindani kweli.

Mondi anajua kuji-brand kuliko Kiba. Pia Mondi ana utajiri wa visa vya kuandikia nyimbo kuliko Kiba. Ndo maana anaweza kutoa ‘hits song’ mara nyingi zaidi ya Kiba. Yaani ile ‘baki tu baki’ na tena zote zikawa za moto.

Ni wazi hata uwezo wa kuandika wa Mondi ni mkubwa zaidi. Na hii ni kutokana na kuanzia muziki wa wachanaji kabla ya kuimba. Ukweli ni kwamba wachanaji wana uwezo wa kuandika kuliko waimbaji.

‘Vesi’ moja ya Fid Q inatoa albamu nzima ya Alikiba. Waimbaji ‘vesi’ zao ni fupifupi zenye kujirudia. Na Mondi anapojisifu kuwa ‘akidili’ na nyimbo za soko la nyumbani pekee, anaweza kutoa hits kila wiki. Ni kweli!

Mondi wa sasa anatazama soko la kimataifa. Ameachana na mtazamo wa Mwananyamala na Bonyokwa.

Lakini Kiba huoni akihangaika na soko la kimataifa. Ni yule yule wa toka Mapenzi Yana Run Dunia hadi Utu na Dodo.

Mondi ni mtu wa kunata na biti la nyakati. Baada ya u-Nigeria kuteka naye akatembea nao. Amapiano kukamata soko akatambaa nalo. Kitu ambacho huwezi kuona kwa King Kiba akirukia vitu vya mpito.

Katikati ya dunia ya Amapiano na Unaijeria. Alikiba yeye akadondoka na pini la Dodo kisha Utu. Nyimbo ambazo hazina muingiliano kabisa na Unaija na Piano. Akakusanya kijiji chake cha Bongo kimya kimya.

Mondi akitaka kuachia wimbo ni lazima atafanya tukio. Na baada ya kuachia ataendelea kutengeneza matukio ya kusukuma pini lake liendelee kukimbizana. Hiki huwezi kuliona kwa Kiba.

Kiba ataachia ngoma ijisambaze  yenyewe. Na mbaya zaidi anaweza kuachia audio bila video. Na huwezi kumuona akihangaika kuisukuma zaidi. Anaacha ijiuze. Kiba ana mashabiki ‘waaminifu’ sana. Akitoa wimbo mashabiki ndo wanapambana kuupaisha. Halafu hajui kama unapendwa na haijali. Huu ni ukatili mtambuka pia.