Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tutarajie nini kufuatia EP ya kwanza kutoka kwa Jux?

Muktasari:

  • Hii ni EP kwa ajili ya kumbukumbu ya ndoa yake na mkewe Priscilla kutokea Nigeria ambaye uhusiano wao ulianza kuonekana mbele ya macho ya umma Julai 2024 na moja ya picha za harusi yao ndio imetumika katika cover la EP hiyo

Dar es Salaam. Staa wa Bongo fleva, Jux ameachia EP yake ya kwanza, A Day To Remember (2025) yenye nyimbo saba ila tatu kati ya hizo zilishatoka awali ambazo ni Si Mimi, God Design na Ex wa Nani wenye mahadhi ya Singeli ikiwa ni mara ya kwanza kufanya aina hiyo ya muziki.

Hii ni EP kwa ajili ya kumbukumbu ya ndoa yake na mkewe Priscilla kutokea Nigeria ambaye uhusiano wao ulianza kuonekana mbele ya macho ya umma Julai 2024 na moja ya picha za harusi yao ndio imetumika katika cover la EP hiyo.

Hatua hiyo inakuja baada ya mkali huyo wa kibao Ololufe Mi (2024), kutoa albamu zake mbili, The Love Album (2019) na King of Hearts (2022) chini ya chapa yake, African Boy iliyoanzishwa kwa mtaji wa Sh400,000, miaka 10 iliyopita.

Kwa ujumla albamu hizo zilifanya vizuri zikimuongezea Jux mashabiki wa ndani na nje hadi kufikisha wafuasi milioni 1 YouTube akiwa ni msanii wa 12 nchini kufikia namba hizo baada ya Diamond Platnumz Harmonize, Rayvanny na Mbosso.

Wengine ni Zuchu, Alikiba, Lava Lava, Nandy, Marioo, Aslay na Rose Muhando, mwanamuziki wa kwanza wa kike Tanzania kusainiwa na lebo kubwa duniani, Sony Music Africa hapo Februari 2012 kisha kitoa kibao chake, Wololo (2013).

Jux anakuja na mradi huo baada ya mwaka uliopita wakali kibao wa Bongo fleva kuachia EP zao, miongoni mwao ni Alikiba (Starter), Rayvanny (ZiiBeats Vol.2), Bwana Misosi (Mbona Kimya), Ibraah (Air Piano), Maua Sama (Sama), Anjella (The Black Queen) n.k.

Sasa tutarajie nini baada ya EP hii kutoka?, haya ni mambo machache tunayoyapa nafasi kubwa kutokana na mtiririko wa kazi wake Jux aliyeibuka kimuziki na kundi la Wakacha lilobamba na wimbo wao, Here We Go (2011). 

Mosi; kolabo zaidi na wasanii wa Nigeria. Kwa sasa Jux ana mashabiki wengi nchini humo baada ya kumuoa mrembo kutokea taifa hilo, Priscilla Ojo ambaye ana nguvu kubwa ya ushawishi, hivyo mwimbaji huyu anatumia nafasi hiyo kufikisha huko muziki wake.

Katika EP hii, Jux amefanya kazi na rapa wa Nigeria, Phyno aliyesikika katika wimbo wake, God Design (2025), akiwa ni msanii wa pili Bongo kushirikiana na Phyno baada ya Rayvanny aliyemshirikisha katika wimbo wake, Slow (2019).

Hivyo basi, kivyovyote vile Phyno hawezi kuwa msanii mwisho Jux kushirikiana naye, kuna wengine watafuata siku sio nyingi maana tayari ana jina huko Nigeria.

Kwa hiyo tusishangae akipita njia za rafiki yake Diamond ambaye ameshirikiana na wasanii wengi wa Nigeria kama P-Square, Davido, Iyanya, Mr. Flavour,  Adekunle Gold, Teni, Tiwa Savage na Rema, mshindi wa MTV VMAs  2023.

Pili; namba kubwa mtandaoni. Kwa mujibu mtandao wa Worldometers, hadi mwaka huu Nigeria ina watu milioni 237.5 ikiongoza kwa Afrika, hili ndilo soko Jux analoliwinda kwa sasa na ndio maana nyimbo zake anachanganya na lugha ya huko.

Kwa hiyo tutarajie kuwa EP hii itapata wasikilizaji wengi sana katika majukwaa ya kidijitali ya kusikiliza muziki kama Boomplay, Spotify, iTunes na YouTube ambapo tayari video zake zimetazamwa zaidi ya mara milioni 325.1. 

Ikumbukwe wimbo wake 'God Design' ulishika namba moja katika chati ya iTunes nchini Nigeria akiwa ni msanii wa pili wa Bongo fleva kufanya hivyo baada ya Diamond kupitia wimbo wake, My Bay (2023) akimshirikisha Chike wa Nigeria pia.

Tatu; tuzo za kimataifa. Kutokana na EP hii tunatarajia itafanya vizuri, basi ni wazi kuwa Jux atashinda tuzo za kimataifa hasa kutokea barani Afrika, na hilo limeonekana tangu alipoanza uhusiano na Priscilla, binti wa mkongwe wa Nollywood, Iyabo.

Baada ya kufanya vizuri na wimbo 'Ololufe Mi 'aliomuimbia mkewe Priscilla ambaye pia alitokea katika video yake, Jux ameshinda tuzo za kimataifa kama Trace zilizofanyika Zanzibar akishinda kama Msanii Bora wa Kiume Tanzania 2024.

Pia alishinda tuzo ya Headies huko Lagos Nigeria, akinyakua kipengele cha Msanii Bora Afrika Mashariki 2025 akiwabwaga wakali kama Bien (Kenya), Diamond Platnumz (Tanzania), Bruce Melodie (Rwanda) na Azawi (Uganda).

Ikumbukwe Jux alishinda Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) 2023 katika kipengele cha Wimbo Bora wa Kushirikiana (Enjoy) akiwa na Diamond ambaye wameshirikiana katika nyimbo nyingine kama Sugua (2019), Enjoy (2023) na Ololufe Mi (2024).

Na video ya wimbo 'Enjoy' ilishatazamwa zaidi ya mara milioni 100 YouTube, hivyo Jux akawa msanii wa nne Tanzania kuwa na video yenye nambo hizo baada ya Diamond (Yope Remix, Inama, Waah!, Jeje na Nana), Harmonize (Kwangwaru) na Zuchu (Sukari).