Usikilizwaji wa ngoma za Diddy wazidi kushuka

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Kushuka kwa uchezwaji wa ngoma hizo redioni kumeripotiwa toka mwezi Novemba mwaka jana wakati Diddy alipofunguliwa kesi ya unyanyasaji wa kingono na aliyekuwa mpenzi wake Cassie.

Orodha ya ngoma za Diddy imeripotiwa kushuka kwa kiasi kikubwa kupigwa kwenye redio, hii ni baada ya kuhusishwa kwenye biashara za ngono.

Kushuka kwa uchezwaji wa ngoma hizo redioni kumeripotiwa toka mwezi Novemba mwaka jana wakati Diddy alipofunguliwa kesi ya unyanyasaji wa kingono na aliyekuwa mpenzi wake Cassie.

Kwa mujibu wa Billboard imeeleza kuwa toka Cassie afungue kesi mahakamani ngoma za Combs zimekuwa zikishuka katika upande wa wasikilizaji na watazamaji ambapo, awali ilizoeleka kuwa nyimbo zake zilikuwa zikifuatiliwa na zaidi ya watu milioni 23.3 lakini sasa ngoma hizo zimeshuka mpaka wafuatiliaji milioni 4 tu.

Uporomokaji huo wa muziki kwa Diddy umeripotiwa kushuka kwa asilimia 88 kwenye uchezwaji redioni na kushuka kwa asilimia 83 kwa wasikilizaji redioni.

Ikumbukwe kuwa Machi 2, makazi ya Diddy ya Los Angeles na Miami yalifanyiwa upekuzi na Mawakala wa Usalama wa Taifa kama sehemu ya uchunguzi wa serikali kuhusu madai ya biashara ya ngono yanayomhusisha msanii huyo.