Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wema Sepetu hajarudia makosa

Muktasari:

  • Septemba 28,  ilikuwa siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa nyota huyo, akitimiza miaka 38, katika siku hiyo aliripotiwa kufanya sherehe na watu wake wa karibu jambo ambalo halijazoeleka.

Dar es Salaam, Mwigizaji mkongwe na mfanyabiashara Wema Sepetu ni kama amejifunza kutokana na yaliyotokea mwaka 2023 katika kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwake, kwani mwaka huu amefanya sherehe ya siri na watu wake wa karibu.

Septemba 28,  ilikuwa siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa nyota huyo, akitimiza miaka 38, katika siku hiyo aliripotiwa kufanya sherehe na watu wake wa karibu jambo ambalo halijazoeleka.

Utakumbuka katika siku ya kuzaliwa ya mwigizaji huyo 2023, alifanya sherehe iliyohudhuriwa na mastaa wengi, lakini iliingia doa baada ya mama yake mzazi kutoa maneno ambayo hayakumpendeza Wema mbele ya wageni waalikwa.

Chanzo cha karibu cha mwigizaji huyo kiliiambia Mwananchi Scoop kuwa Wema alifanya sherehe ambayo alialika watu wake wa karibu akiwemo mpenzi wake Whozu, mwanamitindo Martin Kadinda, msanii Lulu Diva, Zuu 'Mama Steve' mzazi mwenzake Barnaba na wengine wachache.

Hii ni tofauti kwa Wema kwani amezoeleka kufanya sherehe kubwa na kuwaalika watu mbalimbali maarufu huku akijipongeza kwa zawadi za gharama ili kunogesha sherehe zake.