Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Absa yaingia miongoni mwa chapa tano bora

Ofisa Mkuu wa Masoko na Mawasiliano ya Kundi la Absa, Sydney Mbhele.

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa ripoti ya Brand Finance South Africa 2026, thamani ya chapa ya Absa imefikia Rand bilioni 30.6 (Sh 4.83 trilioni) sawa na ongezeko la asilimia 12 ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Johannesburg. Absa Group imetajwa miongoni mwa chapa tatu za benki zenye thamani kubwa zaidi barani Afrika, huku ikiingia katika orodha ya chapa tano bora zenye thamani kubwa zaidi nchini Afrika Kusini katika sekta zote.

Mafanikio hayo yanakuja baada ya thamani ya chapa yake kuvuka Rand bilioni 30 (Sh4.7 trilioni) kwa mara ya kwanza, hatua inayoonesha ukuaji na uimara wa taasisi hiyo katika sekta ya huduma za fedha.

Kwa mujibu wa ripoti ya Brand Finance South Africa 2026, thamani ya chapa ya Absa imefikia rand bilioni 30.6 (Sh 4.83 trilioni) sawa na ongezeko la asilimia 12 ikilinganishwa na mwaka uliopita.

Ripoti hiyo inasema ukuaji huo umeimarisha nafasi ya kundi hilo kama mmoja wa watoa huduma za kifedha wanaoongoza barani Afrika.

Mafanikio haya yanahusishwa kwa kiasi kikubwa na utekelezaji wa mkakati wa “Stori yako ina Thamani,” uliozinduliwa miaka miwili iliyopita kwa lengo la kumweka mteja katika kitovu cha shughuli zote za biashara.

Mkakati huo unazingatia uelewa wa mahitaji ya kibinadamu pamoja na utoaji wa huduma zilizounganishwa na rahisi kutumia.

Utekelezaji wake umeleta mwitikio chanya kutoka kwa wateja, hivyo kuongeza uaminifu, kuimarisha uhusiano na kukuza thamani ya chapa.

Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, Absa imeongeza kasi ya ukuaji wake kwa kuzingatia mahitaji ya wateja, kupanua uwepo wake katika masoko ya Afrika na kuimarisha uwezo wake wa kidijitali pamoja na ubunifu.

Uwekezaji katika mifumo ya teknolojia na huduma za kidijitali umeiwezesha benki hiyo kutoa huduma zilizounganishwa kwa urahisi zaidi, huku ikiendelea kujijengea sifa kama mshirika anayeaminika kwa taasisi mbalimbali.

Ofisa Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Absa, Sydney Mbhele anasema kutambuliwa huko ni uthibitisho wa imani kubwa waliyo nayo wateja pamoja na uimara wa chapa hiyo katika soko lenye ushindani mkali.

Anasema viashiria vya nguvu ya chapa vinaendelea kuimarika, hususan katika kujenga uhusiano wa karibu na wateja kupitia mkakati unaoongozwa na mahitaji yao na teknolojia ya kisasa.

Ripoti hiyo pia inaeleza kuwa chapa imara za benki zina mchango muhimu katika kujenga imani na uthabiti wa uchumi.

Absa imeendelea kujikita katika jukumu hilo kwa kutoa suluhisho bunifu za kifedha zinazowasaidia wateja, taasisi na jamii kukabiliana na mabadiliko ya haraka ya mazingira ya kiuchumi.

Kwa upande wa kifedha, Absa iliripoti ongezeko la asilimia 12 la faida kuu hadi kufikia rand bilioni 24.8.

Mtendaji mkuu anasema matokeo hayo yamechangiwa na kuimarika kwa mapato pamoja na kupungua kwa mikopo chechefu, hali inayoonesha usimamizi madhubuti wa shughuli zake.

Aidha, anasema matumizi ya huduma za kidijitali pia yameongezeka kwa kiasi kikubwa.

“Idadi ya wateja wanaotumia huduma hizo imefikia milioni 3.6, ikiwa ni ongezeko la asilimia 11. Watumiaji hai wa programu ya benki waliongezeka hadi milioni 2.9, huku upakuaji mpya wa programu ukiongezeka kwa asilimia 94 kutokana na maboresho ya huduma na urahisi wa matumizi,” anafafanua.

Absa anasema mafanikio hayo ni msingi wa maendeleo ya baadaye, huku ikiendelea kutekeleza dhamira yake ya kushirikiana na jamii katika kujenga mustakabali imara, jumuishi na wenye fursa zaidi kwa Afrika.