Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fursa nyuma ya unywaji wa kahawa ya ndani

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu akingumza wakati akizindua maandalizi ya tamasha la tano la Kahawa Festival.

Muktasari:

  • Kwa kujibu wa takwimu za Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB), zaidi ya asilimia 93 ya kahawa inayozalishwa nchini, inategemea soko la nje ya nchi huku asilimia saba pekee ndiyo inayotumika ndani ya nchi.

Moshi. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amesema unywaji wa kahawa nchini bado si wa kuridhisha, hivyo ameitaka Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB) kushirikiana na wadau kuwahamasisha Watanzania kupenda kinywaji hicho ili kukuza soko la ndani na kupunguza utegemezi wa soko la nje.

Kwa mujibu wa takwimu za TCB, zaidi ya asilimia 93 ya kahawa inayozalishwa nchini inategemea soko la nje, huku asilimia saba pekee ikitumika ndani ya nchi.

Babu aliyasema hayo Septemba 12, 2024, mjini Moshi wakati akizindua maandalizi ya tamasha la tano la zao hilo, Kahawa Festival, linalotarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia Oktoba 4, 2024.

Tamasha hilo litafanyika katika kiwanda cha kukoboa kahawa cha TCCCO, mkoani Kilimanjaro na kuwakutanisha wadau mbalimbali wa zao hilo.

Babu amesema bado baadhi ya wananchi wana dhana potofu kuhusu unywaji wa kahawa, hivyo elimu inahitajika kutolewa kwa kina ili kuhakikisha inawafikia Watanzania wote, ikiwa ni mojawapo ya jitihada za kukuza soko la ndani la kahawa hadi kufikia asilimia 15 ifikapo mwaka 2025/2026.

“Unywaji wetu wa kahawa sio wa kiwango cha kuridhisha. Nimeambiwa soko la ndani ni asilimia saba tu, na zaidi ya asilimia 90 ya kahawa tunayozalisha inategemea soko la nje. Sasa ni lazima tufanye kazi kubwa ya kuhakikisha wananchi wetu na wakulima wanakunywa kahawa,” amesema Babu. Ameongeza kuwa kuongezeka kwa unywaji wa kahawa nchini, mbali na kukuza soko la ndani, pia kutasaidia jitihada za Serikali kuboresha uchumi wa nchi kwa kuongeza kipato cha wakulima 320,000 kwenye kaya zinazojishughulisha na kilimo cha kahawa na pia kuongeza ajira kwa vijana na kina mama.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa Tanzania (TCB), Primus Kimaryo amesema licha ya Tanzania kuwa mzalishaji mzuri wa kahawa, soko la ndani limeendelea kusuasua.

“Tanzania tunalima kahawa, lakini zaidi ya asilimia 93 inakwenda nje ya nchi. Unywaji wetu bado unasuasua,” amesema.

Ukipita leo mahotelini kote wanakolala wageni, kahawa inayonywewa na wageni haitoi taswira kuwa tunatengeneza kahawa nzuri kiasi hicho,” amesema Kimaryo.

Ameongeza kuwa tamasha la Kahawa, ambalo sasa linafanyika kwa mara ya tano, lilianzishwa ili watengenezaji wa kahawa kama kinywaji waweze kujifunza na kutoa huduma ya kikombe kizuri cha kahawa kwa wageni wanaofika nchini.

Amesisitiza kuwa hatua hiyo pia inatoa fursa kwa wazalishaji wa kahawa nchini, ambao ni wakulima, kuonja kahawa yao, kuijua na kufahamu madhara yanayotokana na utayarishaji wake.

“Kwa kweli, ukikutana na mgeni yeyote, ukimwambia tunalima kahawa, akakwambia hotelini nilipolala sikupata kahawa nzuri, inatuumiza kichwa na ndiyo dhumuni hasa la kuanzisha jambo hili.”

Aidha, Kimaryo aliongeza kuwa tamasha hilo pia lina lengo la kutoa ajira kwa vijana, kwani katika mnyororo wa thamani wa kahawa kuna eneo kubwa ambalo vijana wanaweza kujifunza kutoa huduma, kutayarisha kikombe bora cha kahawa, kujifunza kuonja kahawa, na namna ya kuiandaa, hususani katika hoteli na maduka ya kahawa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Dennis Mahulu amesema wataendesha mashindano mbalimbali katika tamasha hilo, yakiwemo mashindano ya uonjaji wa kahawa, uandaaji wa kahawa bora, pamoja na uzalishaji bora.