Kiwanda chafikisha magari 100 kwa miezi minne

Muktasari:

  • Kiwanda kipya cha cha kutengeneza na kuunganisha magari hapa  Tanzania GF Vehicles Assemblers (GFA) kilichopo Kibaha mkoani Pwani leo kimetengeneza gari la 100 katika kipindi cha miezi minne tangu kilipoanza kufanya kazi Januari 2021.

Kiwanda kipya cha cha kutengeneza na kuunganisha magari hapa  Tanzania GF Vehicles Assemblers (GFA) kilichopo Kibaha mkoani Pwani leo kimetengeneza gari la 100 katika kipindi cha miezi minne tangu kilipoanza kufanya kazi Januari 2021.

Akizungumza leo Alhamisi, Aprili 15, 2021 wakati wa sherehe za kuruhusu gari la 100 kukanyaga ardhini baada ya kuunganishwa tayari kwa  kwa kutembea, Meneja Mkuu wa kiwanda hicho ,Ezra Mereng  amesema ni kazi ngumu ya kuunganisha na kutengeneza magari.


Amesema changamoto ni nyingi kutokana na kutokuwa na wataalamu wengi katika sekta hii ya magari lakini kwa kushirikiana na wataalamu wa nje  waliunganisha magari 10 ya awali na baadae wakaondoka na wakabaki Watanzania waliofikisha magari 100 katika kipindi cha miezi minne.

Mereng ameziomba tasisisi za Serikali kuagiza magari yasiyounganishwa ili kazi ya kuunganisha ifanywe na viwanda vya ndani kwa ajili ya kukuza pato la taifa na kupanua wigo wa ajira

Kiwanda hicho kimeajiri wafanyakazi 100 ambao ni pamoja wenye ajira za kudumu, mikataba ya muda mfupi na vibarua,