Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Madebe yawaminya walima ufuta

Muktasari:

Sheria ya Vipimo inawataka wakulima kutumia mzani katika mauzo ya mazao yao, lakini wengi hutumia madebe.

Dodoma. Wakulima wa ufuta nchini wameshindwa kunufaika na mapato yatokanayo na zao hilo kutokana na kutumia vipimo visivyo sahihi, imeelezwa.

Sheria ya Vipimo inawataka wakulima kutumia mzani katika mauzo ya mazao yao, lakini wengi hutumia madebe.

Akizungumza mjini Dodoma jana, Mratibu wa mradi huo Wilaya za Bahi na Manyoni kutoka Taasisi ya Inades Formation Tanzania, Baruani Baruani alisema wakulima wamekuwa wakitumia madebe kuuzia wanunuzi, jambo ambalo linawapunja.

“Wakulima wana matumizi yasiyosahihi ya vipimo, baada ya kuwapatia mafunzo tunategemea wauze kwa kutumia mzani. Wilaya za Bahi mkoani Dodoma na Manyoni Singida wanatumia madebe ambayo hayazingatii uzito unaosahihi,” alisema Baruani.

Hata hivyo, Baruani alisema kupitia Mradi wa Ufuta unaoendeshwa na Inades kwa kushirikiana na Shirika la Farm Afrika, unalenga kuwawezesha wakulima kutumia vipimo sahihi.

Meneja Mradi wa Ufuta kutoka Shirika la Farm Africa, Tumaini Mkenge alisema licha ya kutoa elimu kwa wakulima wa ufuta kwa njia ya shamba darasa, wameanzisha mafunzo ya Teknolojia ya Habari (Tehama) kupitia simu za mkononi.

Alisema chini ya mafunzo hayo watawezesha wakulima kutumia teknolojia ya Tehama kuwafundisha wenzao kupitia mada zitakazotolewa na wataalamu kupitia simu hizo.

“Chini ya utaratibu wa Tehama, tunararajia kuwafikia wakulima wengi zaidi wa ufuta,” alisema.

Mkulima wa Kijiji cha Mwitikila wilayani Bahi, Keneth Mwanza alisema awali alikuwa akiambulia debe tatu anapolima eka moja, lakini baada ya kufuata maelekezo ya wataalamu anapata zaidi ya magunia mawili na nusu.

Ofisa wa Uwezeshaji wa Shirika la Farm Africa, Josh Meek alisema mafunzo ya Tehama yamefanyika pia nchi za Ethopia na Kenya, ambako yameonyesha mafanikio.

“Kupitia ICT wakulima watatumia simu zao kupata elimu ya masoko na namna ya kutunza mashamba yao kitaalamu, tayari mafanikio yameanza kuonekana,” alisema Meek.