Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mikopo ya simu janja ilivyobadili maisha ya wajasiriamali wadogo

Picha na Mtandao.

Dar es Salaam. Mikopo ya simu janja inaendelea kubadilisha maisha ya Watanzania wengi, hususan wajasiriamali wadogo na wafanyakazi wa sekta isiyo rasmi, kwa kuwawezesha kuongeza kipato na kupanua masoko kupitia majukwaa ya kidijitali.

Juma Mbunda (28), dereva wa bodaboda kutoka Kitunda, simu janja imekuwa chombo muhimu cha kazi badala ya kuwa kifaa cha mawasiliano pekee. Kabla ya kupata simu hiyo, Juma alitegemea wateja wa kupita na wa eneo lake, hali iliyomfanya kutumia muda mwingi kusubiri abiria.

“Mabadiliko yalianza baada ya kuchukua simu kwa mkopo. Nilianza kupokea simu za wateja moja kwa moja na kutumia ramani kujua maeneo,” anasema Juma.

Anasema ndani ya miezi mitatu, mapato yake yaliongezeka kutokana na wateja kumtafuta moja kwa moja na kupunguza gharama za mafuta. Hatua kubwa zaidi ilikuja alipojiunga na huduma za usafiri mtandaoni, jambo lililomfungulia soko pana zaidi.

Hadithi kama hiyo inaonekana kwa Neema Kamunga (21), mfanyabiashara wa nguo kutoka Mpanda. Baada ya kupata simu janja kwa mkopo, alianza kutumia mitandao ya kijamii kutangaza bidhaa zake.

“Nilianza kuposti picha na video za nguo kila siku, na wateja wakaanza kuwasiliana nami moja kwa moja,” anasema Neema.

Ndani ya miezi michache, mauzo yake yaliongezeka kwa kiasi kikubwa, huku wateja wapya wakitoka nje ya eneo lake la biashara.

Takwimu zinaonyesha matumizi ya simu na intaneti nchini yanaendelea kuongezeka kila mwezi, hali inayoonyesha umuhimu wa teknolojia katika shughuli za kiuchumi.

Kampuni za simu kama huunganishwa na mifumo ya fedha kwa simu ili kurahisisha malipo na kupanua upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wafanyakazi wa sekta isiyo rasmi.

Mathalani kampuni ya Airtel Tanzania kwa kushirikiana na itel Mobile unawaruhusu wateja kununua simu kama itel A70 na itel A50 kwa kulipa kidogo mwanzoni na kumalizia kwa awamu za wiki au mwezi. Simu hizi huja na vifurushi vya data vinavyowawezesha watumiaji kuanza kutumia huduma za kidijitali.

Mchambuzi wa masuala ya uchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Dk Bravious Kahyoza alisema simu janja zinapanua soko la biashara na kuongeza ufanisi wa kazi.

Dk Kahyoza alisema simu janja si anasa tena katika miji na maeneo ya pembezoni mwa miji nchini Tanzania. Ni zana muhimu kwa wajasiriamali wadogo, madereva wa bodaboda na wafanyakazi wa sekta isiyo rasmi.