Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

TRA, viongozi wa dini wahimiza ulipaji kodi kwa hiari

Viongozi kutoka madhehebu mbalimbali ya Dini wakiwa  kwenye   kongamano la Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) linalohusu maadili  katika ukusanyaji kodi lililifanyika jijini Dar es Salaam

Muktasari:

  • TRA imekutana na viongozi hao wa dini katika kongamano ikiwa ni moja ya njia katika kuifikia jamii.

Dar es Salaam. Viongozi wa dini wamewahimiza wananchi kutosita kulipa kodi kwani kufanya hivyo ni sehemu ya ibada ambayo dini zote zinahimiza hilo.

Hayo yamesemwa leo Jumatano Juni 17, 2026 na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), Sheikh Alhad Mussa Salum kwenye kongamano la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na viongozi wa dini kuhusu maadili katika ukusanyaji kodi lililofanyika jijini Dar es Salaam.

Sheikh Alhad amesema katika suala kodi kwa yule anayekusanya na anayetoa ni watu wawili wanashirikiana katika kheri.

"Ulipaji kodi tunasema ni ibada kwa kuwa katika moja ya mambo anayoyapenda Mwenyezi Mungu ni kukusanya kodi hivyo yule anayekwenda kukusanya na yule anayetoa wote wajue wanafanya Ibada na wameshirikiana katika kheri," amesema.

Amesema watu wasifike mahali wakaona TRA inapofika kwao ni kama  wametembelewa na Israeli mtoa roho, bali ni kodi ambayo itarudi kwa maskini na mafukara ikiwemo  kuwezesha kujenga vituo vya afya, shule, barabara na kuleta umeme.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), Sheikh Alhad Mussa Salum, akizungumza kwenye kongamano la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na viongozi wa dini kuhusu maadili  katika ukusanyaji kodi lililifanyika jijini Dar es Salaam.

"Mwenyezi Mungu hakutupa hizi mali kwa kutuachia tu kwani vyote ni milki zake ikiwemo sisi na alichofanya ni kutuwekea mamlaka za kusimamia hayo mambo.

"Kikubwa hapa ni mtoa kodi na mchukuaji kodi wote wawe waadilifu kwa kuwa ukiwa unaona wewe unaonewa katika kutoa kodi hata biashara yako unayoifanya haiwezi kuwa na baraka," amesema Sheikh Alhad.

Naye Mwenyekiti wa JMAT Mkoa wa Dar es Salaam, Mchungaji Christosiler Kalata, amesema hata kwenye biblia kumehimizwa ulipaji kodi na kinachofanywa na TRA ni utekelezaji wa kile kilichoandikwa katika kitabu hicho cha Mungu.

Pia ametaka kutolewa elimu juu ya faida ya kodi na jinsi zinavyotumika hali itakayowezesha watu wengi kulipa kodi bila usumbufu mkubwa.

Viongozi kutoka madhehebu mbalimbali ya Dini wakiwa  kwenye   kongamano la Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) linalohusu maadili  katika ukusanyaji kodi lililifanyika jijini Dar es Salaam

"Kwa upande wa wale wakusanyaji wa kodi nao waboreshewe marupurupu badala ya kukwapua kwani mtu umemuweka kwenye kukusanya kodi, lakini humpi marupurupu yoyote mwisho lazima akwapue tu kwa wananchi," amesema.

Kiongozi mkuu waumini wa dhehebu la Shia, Sheikh Hemed Jalala, amesema amepongeza hatua ya TRA kuwakutanisha viongozi hao wa madhehebu mbalimbali.

Sheikh Jalala amesema kwa kuwa kuanzia Ijumaa, Jumamosi na Jumapili wapo Watanzania wanaokuwa kwenye mdhabahu yao, hivyo wao wakiweza kuelewa umuhimu wa kulipa kodi na kuwaeleza waumini wao  hakuna atakayepinga hilo.

Awali, Naibu Kamishna Mkuu wa TRA, Mcha Hassan Mcha, amesema mamlaka hiyo inatambua umuhimu wa maadili katika jamii kwani dini zote zinahimiza katika haki, kuheshimu sheria na mamlaka na kutanguliza Taifa mbele.

kwenye kongamano la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na viongozi wa dini kuhusu maadili katika ukusanyaji kodi lililifanyika jijini Dar es Salaam

Mcha amesema wananchi wanapolipa kodi wanachangia huduma mbalimbali za kijamii zinazotolewa na serikali na kueleza nia ya TRA ni kuhakikisha wananchi wanalipa kodi kwa kufuata sheria haki na bila mabavu.

"Pamoja na kutakiwa kufanya haya yote, TRA inatambua msingi imara wa taasisi ni maadili ambapo naahidi tutaendelea kutumia njia mbalimbali kuhakikisha hilo linatekelezwa kivitendo.

Akieleza kuhusu mafanikio, amesema kupitia kuimarika kwa mifumo ya usimamizi, nidhamu ya kazi, matumizi ya Tehama na ushirikiano wa walipakodi, TRA imeendelea kupata mafanikio chanya katika ukusanyaji wa mapato.

Mei 2026 pekee, amesema Tanzania Bara ilikusanya Sh2.96 trilioni sawa na asilimia 104.4 ya lengo, ikilinganishwa na Sh2.40 trilioni zilizokusanywa katika kipindi kama hicho mwaka uliopita 2025.

"Mafanikio haya yanaonesha wazi kuwa pale ambapo uadilifu, uwajibikaji na ushirikiano vinapopewa kipaumbele, matokeo chanya hupatikana," amesema Mcha.

Hata hivyo, ameeleza  kuwa wamepokea mawazo yote yaliyotolewa na viongozi hao wa dini  na kuahidi kuendelea kushirikiana zaidi na kuona kila Mtanzania analipa kodi kwa hiari.