Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wajasiriamali wachangamkia fursa mkutano wa Samia Mbeya

Muktasari:

  • Kwa sasa shughuli inayoendelea ni wasanii mbalimbali kutumbuiza wakati akisubiriwa mgombea urais wa CCM, Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya mkutano wa kampeni.

Mbeya. Wananchi na makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya wamejitokeza kwa wingi kuhudhuria mkutano wa mgombea urais wa Chama hicho, Samia Suluhu Hassan.

Mgombea huyo ambaye pia ni Rais wa sasa, anatarajia kufanya mikutano minne mkoani hapa baada ya kumaliza ziara yake mkoani Songwe jana Septemba 3, 2025.

Kiongozi huyo akiwa mkoani hapa ataanza na mkutano mdogo katika mji wa Mbalizi, kisha mkutano mkubwa viwanja vya Old Airport kwa siku ya leo.

Ziara ya mgombea huyo inatarajia kuendelea kesho Septemba 5, 2025 kwa mkutano mdogo mji wa Tukuyu kisha kuhitimisha wilayani Mbarali kwa mkutano mkubwa wa kampeni.

Hadi sasa wananchi wameonekana kujitokeza kwa wingi huku makundi mbalimbali yakimsubiri kiongozi huyo.

Wajasiliamali nao ni sehemu ya wananchi waliofika viwanjani hapo wakiwa na bidhaa zao kwa ajili ya kupata chochote kwa maisha yao.

Kuhusu ulinzi na usalama, Jeshi la Polisi limeonekana kuwa imara huku ukaguzi kwa wanaoingia getini nao ukiendelea kuhakikisha kila mmoja anashiriki na kumaliza salama tukio hilo.


Endelea kufuatilia Mwananchi Digital kwa habari zaidi.