Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wanawake wabeba uchumi wa buluu, lakini wanabaki pembeni katika maamuzi

Wadau mbalimbali wa maendeleo wilayani Babati mkoani Manyara ambao wameshiriki kupanda miti 5,000 kwa ajili ya kuhifadhi mazingira na kutunza mapito ya wanyamapori (shoroba)

Muktasari:

  • Licha ya kuwa nguvu kazi kuu katika shughuli za uchumi wa buluu, wanawake bado wanakosa nafasi katika maamuzi muhimu, hali inayotajwa kuwa kikwazo kikubwa kwa maendeleo endelevu ya maeneo ya pwani.

Tanga. Wanawake katika uchumi wa buluu bado wako nyuma katika ngazi za maamuzi licha ya mchango wao mkubwa, hali inayohitaji mabadiliko ya sera na mifumo.

Hoja hiyo iliibuliwa katika kongamano la maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani 2026, ambapo wadau walisisitiza umuhimu wa kuwapa wanawake nafasi zaidi katika maamuzi.

Mkurugenzi wa Mradi wa ReSea, Perpetua Angima, alisema wanawake wanashiriki kikamilifu katika shughuli za baharini kama kilimo cha mwani, uchakataji wa samaki na ufugaji wa viumbe wa baharini, lakini hawana ushawishi kwenye maamuzi.

Evansia Shirima kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais alisema Sera ya Taifa ya Uchumi wa Buluu ya 2024 inalenga kuongeza ushiriki wa wanawake, ingawa mabadiliko ya tabianchi bado yanawaathiri zaidi.

Kwa upande wa wanufaika, Jamila Ali alisema mafunzo yameongeza ujuzi na uzalishaji, lakini changamoto kama mitazamo hasi, ukosefu wa mitaji na miundombinu duni bado zipo.

Wadau walisisitiza kuwa bila kuwapa wanawake nafasi ya kushiriki kikamilifu katika maamuzi, maendeleo ya uchumi wa buluu hayatakuwa endelevu.