Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Watoa huduma za bima wapewe somo la ubunifu

Muktasari:

  • Kwa kufanya hivyo kumetajwa kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma mbalimbali za bima nchini

Dar es Salaam. Watoa huduma za bima nchini Tanzania wametakiwa kubuni bidhaa bora, huku wakisisitizwa kufanya malipo ya madai ya wateja kwa wakati.

Wito huo umetolewa leo Jumanne, Mei 20, 2023 jijini Dar es Salaam na Naibu Kamishna Mamlaka ya Usimamizi wa Bima (Tira), Khadija Said wakati wa hafla ya uzinduzi wa bima ya maisha ya Akiba Flex Plan kutoka Kampuni ya Bima ya Jubilee Life Insurance.

Khadija amesema watu wanapokata bima huwa na malengo mbalimbali hivyo madai yao yanapolipwa kwa wakati huwasaidia kutimiza malengo yao kwa haraka.

"Watoa huduma za bima mjitahidi sana kulipa mafao kwa wakati kama mnavyowahimiza na kuwaunganisha wateja katika huduma zenu," amesisitiza.

Pia, amesisitiza watoa huduma hao kuzingatia maadili na kujiepusha na vitendo vya udanganyifu kwani unapunguza ufanisi na uendelevu wa huduma zinazotolewa.

"Ninawasisitiza mnavyotoa huduma kwa wananchi kuwa waaminifu na waadilifu ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za bima," amesema.

Vilevile ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa sekta ya bima kushirikiana na Serikali kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kujiunga na huduma za bima na namna gani zitawahakikishia ulinzi wa maisha.

Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu kutoka Kampuni ya Bima ya Jubilee Life Insurance, Hellena Mzena amewahimiza Watanzania kujiunga na bidhaa mbalimbali za bima ili kujihakikishia ulinzi na utatuzi wa changamoto mbalimbali zinapowakabili.

Amesema si huduma ya kifedha pekee bali ni ahadi ya ulinzi, utu pamoja na amani ya moyo.

"Mfano wa huduma ya bima tuliyoizindua inayomuwezesha mteja kuwekeza pesa ili kutimiza malengo mbalimbali ya maisha huku ikitoa nafasi ya mteja kutoa mafao yake hadi mara tatu kabla ya muda ya ukomo wa bima kuisha," amesema Mzena.