Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

WHI yavuka lengo la mauzo ya vipande

Muktasari:

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Nyumba na Uwekezaji ya Watumishi (WHI), Dk Fred Msemwa amesema wameuza vipande vya Mfuko wa Faida Fund vya Sh12.95 bilioni tofauti na malengo yaliyowekwa ya kuuza Sh7 bilioni.

Dar es Salaam. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Nyumba na Uwekezaji ya Watumishi (WHI), Dk Fred Msemwa amesema wameuza vipande vya Mfuko wa Faida Fund vya Sh12.95 bilioni tofauti na malengo yaliyowekwa ya kuuza Sh7 bilioni.

Mfuko mpya wa uwekezaji wa pamoja wa Faida Fund unaosimamiwa na WHI ulianzishwa Novemba mwaka 2022 unawezesha na kuruhusu wawekezaji wenye mitaji midogo kuwekeza.

Leo Alhamisi Januari 12, 2023 akitoa taarifa ya mwenendo wa mfuko ulianza kufanya kazi Novemba Mosi 2022, Ofisa  Mtendaji Mkuu wa WHI, Dk Fred Msemwa amesema wamefikia lengo kwa vipande walivyoviuza kuanzia Novemba Mosi hadi Desemba 31, 2022.

Dk Msemwa amesema baada mfuko huo kuanza kufanya kazi walitarajia kuuza vipande vya Sh7.5 bilioni, lakini zimepatikana Sh 12.95 sawa na asilimia 173.

"Tumevuka malengo tuliyoyaweka, tunawashukuru wote waliowekeza na mfuko huu unakua kwa kasi, hadi sasa waliojindikisha ni 3,800 na waliowekeza ni 800.

"Wawekezaji wa mfuko huu wamekuwa na imani na WHI, tunawahidi tutafanya kazi kwa bidii katika utekelezaji wa majukumu yetu," amesema Dk Msemwa.