Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Trump alimuahidi Kim Jong lifti ya ndege

Trump alimuahidi Kim Jong lifti ya ndege

Muktasari:

  • Donald Trump alimuahidi kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un kumpa lifti katika ndege maalum ya rais wa Marekani, maarufu kwa jina la Air Force One, ili kumrudisha nchini kwake mara baada ya mkutano wa wawili hao uliofanyika Hanoi miaka miwili iliyopita, kwa mujibu wa makala ya BBC.

Seoul, Korea Kusini (AFP). Donald Trump alimuahidi kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un kumpa lifti katika ndege maalum ya rais wa Marekani, maarufu kwa jina la Air Force One, ili kumrudisha nchini kwake mara baada ya mkutano wa wawili hao uliofanyika Hanoi miaka miwili iliyopita, kwa mujibu wa makala ya BBC.
Kwanza Kim na Trump waliingia katika vita ya maneno na vitisho, kabla ya harakati za kidiplomasia kukubaliana kikao cha wawili hao huku rais huyo wa zamani wa Marekani akimtangazia mwenzake upendo.
Lakini hakukuwepo na maendeleo yoyote ya maana baada ya kikao hicho, huku mpango huo ukikwama kutokana na ulegezaji vikwazo na kile ambacho Korea Kaskazini ilikuwa tayari kutoa kwa kulegezewa vikwazo.
Kwa mujibu wa makala hiyo ya BBC inayoitwa "Trump Takes on the World", rais huyo wa zamani wa Marekani alistua hata wanadiplomasia waandamizi kwa kutoa ahadi hiyo ya kumpa Kim Jong lifti ya ndege ya Air Force One kumrejeshwa kwao baada ya kikao hicho cha mwaka 2019 nchini Vietnam.
Kama Kim angekubali, kitendo hicho kingemuweka kiongozi huyo wa Korea Kaskazini -- na inawezekana baadhi ya watu katika msafara wake -- ndani ya ndege maalum ya rais wa Marekani ambayo ingeingia anga la Korea Kaskazini, ikiibua maswali kadhaa ya kiusalama.
Lakini Kim alikataa.
"Rais Trump alitaka kumpa Kim lifti ya ndege ya Air Force One kurejea nyumbani," Matthew Pottinger, mtaalamu mwandamizi wa Baraza la Usalama wa Taifa la Trump, aliiambia BBC katika makala hiyo ya mwishoni mwa wiki.
"Rais alijua kuwa Kim aliwasili Hanoi kwa treni iliyosafiri kwa zaidi ya siku moja ikipitia China kwenda Hanoi na akasema: 'naweza kukurejesha nyumbani kwa saa mbili kama ukitaka'. Kim alikataa."
Kwa ajili ya mkutano wake wa kwanza na Trump uliofanyika Singapore mwaka 2018, Kim alitumia ndege ya Air China.
Wakati wa mkutano huo wa wawili hao nchini Singapore, Trump alimuonjesha Kim kwa kumuonyesha jinsi kulivyo ndani ya gari la rais wa Marekani -- aina ya Cadillac la thamani ya dola 1.5 milioni na ambalo pia linajulikana kama "The Beast" -- katika tukio linaloonekana la kuonyeshana urafiki mpya.
Lakini mwezi uliopita, Kim alisema Marekani ndio adui yake namba moja katika masuala ya silaha za nyuklia, akisema sera ya Marekani kuhusu taifa lake haitabadilika milele bila ya kujali nani yuko madarakani.