Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‘Yesu’ wa Tongaren aitwa polisi kwa mahojiano

Kiongozi wa kiroho wa Kanisa la New Jerusalem sect lililopo Bungoma nchini Kenya, Eliud Simiyu.

Muktasari:

  • Mhubiri na kiongozi wa dhehebu la New Jerusalem, Eliud Wakesa ametakiwa kuripoti kwa maafisa wa Polisi kwa mahojiano na upelelezi kuhusu mahubiri yake.

Kenya. Mhubiri na kiongozi wa dhehebu la ‘New Jerusalem,’ Eliud Wakesa maarufu kama ‘Yesu wa Tongaren’ ametakiwa kuripoti kwa maafisa wa Polisi kwa mahojiano na upelelezi kuhusu mahubiri yake. Redio ya Kimataifa ya Ufaransa (RFI) rimeripoti.

 Hatua hiyo imekuja baada ya Rais wa Kenya William Ruto kuunda Tume ya Uchunguzi dhidi ya vifo vya watu zaid ya 100 vilivyotokea msitu wa Shakahola uliopo eneo la Pwani ya Kenya katika Kaunti ya Kilifi.

Aidha kitendo cha Wakesa kuitwa kwenye mahojioano kimetokana na mahubiri yake ambayo alijitangaza kwa waumini wake kuwa yeye ndiye Yesu wa Tongaren na ana malaika wake wanaomsaidia katika kazi zake kama mwana wa Mungu.

Taarifa zinasema Wakesa ametakiwa kufika Polisi leo Mei 10, 2023 kwa ajili ya kufanyiwa mahojiano kuhusu mafundisho yake ya kidini yanayotiliwa shaka kwa watu wengine.

Kwa upande wake Wakesa amesema hana hatia yeyote ya kutakiwa kuhojiwa na Polisi na hajafanya kosa lolote zaidi sana amesisitiza kuwa yeye anafanya kazi ya kueneza injili kwa viumbe waliopotea.

Wakati huohuo kwa mujibu wa Tovuti ya Taifa Leo ya nchini humo imesema Serikali imetuma notisi ya siku 30 kufuta kanisa la New Life Prayer Centre and Church la Mchungaji Ezekiel Odero na Good News International la mhubiri Paul Mackenzie.

Akizungumza mbele ya kamati mahsusi katika tume inayochunguza vifo tata Shakahola, msajili wa mashirika ya kijamii Jane Joram amesema makanisa hayo yanalengwa kwa sababu yamehusishwa kwa njia moja au nyingine na sakata linaloendelea.


Imeandaliwa na Dorcas Hhando