Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

‘Yesu wa Tongaren’ ajisalimisha polisi kuokoa maisha yake, waumini wamvizia

Kiongozi wa kiroho wa Kanisa la New Jerusalem sect lililopo Bungoma nchini Kenya, Eliud Simiyu.

Muktasari:

  • Kiongozi wa kiroho wa Kanisa la New Jerusalem sect lililopo Bungoma nchini Kenya, Eliud Simiyu maarufu ‘Yesu wa Tongaren’ amelazimika kwenda kutoa taarifa polisi ili kuokoa uhai wake baada ya waumini wake kuapa kumsulubisha msalabani itakaopojiri Ijumaa Kuu siku ambayo Yesu aliteswa msalabani.

Kenya. Kiongozi wa kiroho wa Kanisa la New Jerusalem sect lililopo Bungoma nchini Kenya, Eliud Simiyu maarufu ‘Yesu wa Tongaren’amelazimika kwenda kutoa taarifa polisi ili kuokoa uhai wake baada ya waumini wake kuapa kumsulubisha msalabani itakaopojiri Ijumaa Kuu siku ambayo Yesu aliteswa msalabani.

Simuyu amefikia hatua hiyo kutokana na waumini wa kanisa lake kutaka kumsulubisha kama mfano wa mateso ya Yesu Kristo jambo ambalo amelipinga na kuripoti polisi ili kuokoa maisha yake.

Mtu huyo ambaye anajita ‘Yesu wa Tongaren’ hajui hatima ya maisha yake kutokana na ahadi walizoweka wakazi wa Bungoma wanaosali katika kanisa lake.

Wananchi hao wanaamini kutokana na kujiita jina hilo, wameeleza kuwa kama Yesu alivyosulubiwa na mafarisayo, kuzikwa na kufufuka siku ya tatu, nao wanaamini atapitia hatua hiyo kisha kupaa mbinguni.

“Yesu wa Bungoma sasa amelalamika kuwa maisha yake yapo hatarini kuuawa kwenye Pasaka hii inayokuja. Hii ni kutokana na kuwasikia wakazi wa Bungoma wakisema anatakiwa kusulubiwa vilevile kama Yesu. Wananchi wa eneo hilo wamekuwa na imani ya kwamba ni Mungu wa kweli na wana imani atafufuka siku ya tatu na kupaa mbinguni kwa hiyo aache wasiwasi wake.

Simiyu ni mwanzilishi na kiongozi wa Kanisa la Yerusalem ambalo makuu yake ni Kijijiji cha Lukhokwe Jimbo la Tongaren.

Awali, alijitangaza kuwa yeye ni Yesu halisi anayetajwa kwenye Biblia na ana uwezo wa kufanya miujiza.

Waumini wanaosali katika kanisa hilo wana utamaduni ya kujiita majina ya manabii au malaika, huku wakizuiwa kujiita majina yao halisi.

Simiyu alizaliwa mwaka 1981 na wazazi wake wanafahamika kwa majina Francis na Cecilian Simiyu hata hivyo walifariki akiwa bado mdogo.

Kiongozi huyo wa kanisa, alizaliwa akiwa katika imani ya Kikatolii na alisoma Shule ya Msingi Mukuyu Tongaren, Kaunti ya Bngoma.

Hata hivyo aliacha shule akliwa kidato cha kwanza kisha kuanza kujishughulisha na kilimo.

Alifanikiwa kuoa akiwa na miaka 20, ambapo mwaka 2001.

Simiyu ni baba wa watoto wanane na mtoto wake mkubwa anasoma chuo cha ufundi Kaunti ya Kiambu na mtoto wake wa pili ameshajiunga na masomo ya chuo kikuu.

Mwaka 2009, Simiyu baada ya mtafaruku wa kifamilia kutokea  alipelekwa hospitali kwa mujibu wa majirani zake. Tangu alipotoka hospitali ndipo alianza kuhubiri.