Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Vilio, simanzi vyatawala KCMC ndugu wakishuhudia majeneza 36 yakiwasili

Muktasari:

  •  Mpaka sasa vifo vilivyokana na ajali ya barabarani vimefikia 42 huku majeruhi wawili waliosalia katika hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini, KCMC wakiendelea na matibabu baada ya wengine 24 kuruhusiwa.

Moshi. Vilio na simanzi vimetawala katika viwanja vya Hospitali ya KCMC, mkoani Kilimanjaro wakati ndugu wakishuhudia majeneza 36 kati ya 42 yenye miili ya ndugu zao waliofariki dunia ajalini baada ya magari mawili kugongana na kuwaka moto Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro. 

Ndugu hao pamoja na waombolezaji wengine ambao wameanza kuwasili saa 3 asubuhi ya leo Alhamisi, Julai 3, 2025 katika viwanja hivyo wameshindwa kujizuia huku wakibubujikwa na machozi baada ya kuona majeneza yenye miili ya ndugu zao yakishushwa kwenye magari ya polisi.

Hata hivyo, kutokana na wingi wa majeneza, miili hiyo imekuwa ikiletwa awamu kwa awamu katika viwanja hivyo kwa ajili ya taratibu ya kuaga na kisha kukabidhiwa kwa ndugu.

Kila majeneza yalipokuwa wakishushwa katika magari na kwenda kuwekwa eneo maalumu lililoandaliwa, vilio kutoka kwa waombolezaji viliongezeka. 

Ajali hiyo ilitokea Juni 28, 2025 katika eneo la Sabasaba, Same mjini ikihusisha basi Kampuni ya Chanel One lililokuwa likitokea Moshi kwenda Tanga na basi dogo aina ya Coaster lililokuwa likitokea Same Mjini kwenda Moshi kugongana uso kwa uso.

Baada ya kugongana, magari yote mawili yaliwaka moto, yakiwa na abiria ndani.

Mpaka sasa vifo vilivyokana na ajali hiyo vimefikia 42, huku majeruhi wawili waliosalia katika Hospitali ya KCMC wakiendelea na matibabu baada ya wengine 24 kuruhusiwa.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Viongozi mbalimbali wa serikali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Nurdin Babu, wakuu wa wilaya za mkoa huo, wabunge wanaomaliza muda wao na wagombea wengine wa nafasi za ubunge katika majimbo mbalimbali ya Mkoa wa Kilimanjaro wamewasili katika viwanja hivyo kwa ajili ya shughuli ya kuaga miili ya wapendwa hao.

Katika viwanja hivyo, ipo familia moja iliyopoteza watu 10, wakiwemo ndugu wanne na wapangaji sita ambao pia wanaangwa katika viwanja hivyo.

Baada ya miili hiyo kuagwa kwa ibada maalumu, itakabidhiwa ndugu na kuanza safari kuelekea wilayani Same, kuwapumzisha ndugu zao hao katika makazi yao ya milele.

Miili hiyo itakabidhiwa kwa ndugu baada ya kukamilika kwa vipimo vya vinasaba (DNA).


Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi.