Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Kenya azuiwa kuingia Marekani

Mwanasheria Mkuu wa zamani wa Serikali ya Kenya (AG), Amos Wako

Muktasari:

  • Marekani imemzuia mwanasheria mkuu mstaafu wa Kenya kutoingia nchini pamoja na familia yake.

Nairobi, Kenya. Mwanasheria Mkuu wa zamani wa Serikali ya Kenya (AG), Amos Wako amepigwa marufuku kuingia na kufanya bishara na Marekani.

Aidha, nchi hiyo pia imezuia familia yake akiwamo mkewe, Flora Ngaira na mtoto wake wa kiume, Julius Wako.

Taarifa ya waziri wa Mambo ya nje wa Marekani kwa vyombo vya habari ilisema kuwa mwanasheria huyo ambaye sasa ni Seneta wa Kaunti ya Busia imezuia kuingia katika nchi hiyo kutokana na kuhusika na vitendo vya rushwa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na waziri Michael Pompeo, Wako anadaiwa kuhusika katika vitendo hivyo akiwa katika nafasi yake ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

“Hii ina maana kwamba Wako, mkewe na mtoto wake hawataruhusiwa kuingia nchini Marekani au kujihusisha na biashara katika kampuni yoyote ya nchi hiyo.

 “Leo Jumatatu (jana), idara imemzuia mwanasheria wa zamani wa Kenya, Amos Sitswila Wako kutokana na kujihusisha kwake na vitendo vya rushwa,” alisisitiza waziri huyo kupitia taarifa yake iliyotolewa jana jioni.

Pompeo alisema uamuzi huo umefikiwa kupitia   kifungu Sheria ya Idara ya Nchi, Operesheni za Kigeni na za matumizi ya mipango ya mwaka wa 2019 (Div. F, P.L. 116-6), kama inavyotekelezwa na Sheria ya Idara ya Ardhi, 2020 (Div. A, P.L. 116-59).

Alisema kifungu cha 7031 (c) kinampa mamlaka waziri wa Mambo ya nje kuwachukulia hatua maafisa wa serikali za nje waliohusika katika ufisadi mkubwa pamoja na familia zao kuwazuia kuingia Marekani.

Hata hivyo, waziri huyo alisema Marekani itaendelea kusimama na Wakenya wote wa vita ddidi ya vitendo vya rushwa na ufisadi.