Australia kupiga kura wenyeji kupewa kipaumbele umiliki wa rasilimali
Waziri Mkuu wa Australia, Anthony Albanese akiongoza wananchi wanaotaka wenyeji wapewe kipaumbele
Australia. Wananchi wa Australia Oktoba 14, 2023 wanatarajia kupiga kura za kupitisha mpango wa wazawa wan chi hiyo kuwa na nguvu zaidi ya kulishuri bunge na sera zao kusikilizwa hasa katika umiliki rasilimali.
Endapo raia milioni 17 wa nchi hiyo wenye vigezo vya kupiga kura wakilipitisha azimio hilo, Katiba ya nchi hiyo iliyowahi kuwa koloni la Uingereza itabadilika na kuwekwa sehemu hiyo ya ‘sauti ya wenyeji’.
Wakati wanaopigia chapuo mpango huo wakisema utaenda kuleta tija kwa wananchi wazawa na maendeleo yao lakini wengine wamekosoa huku wakisema ni dalili ya kugawanyika kwa umoja wa kitaifa.
Wanasiasa wan chi hiyo wamegawanyika katika kuunga mkono jambo hilo huku Waziri Mkuu wan chi hiyo, Anthony Albanese akipigia chapuo suala hilo.
Msukumo huo unakuja baada ya wenyeji wan chi hiyo wengi kuona fursa zinachukuliwa na watu wan je huku wao ambao kiasili ni watu wa visiwa vya Torres Strait Islander wakiendelea kuwa maskini na kukosa fursa.