Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

British Council kufunga ofisi Tanzania, sababu yatajwa

Picha na Mtandao.

Muktasari:

  • Hatua hiyo ni sehemu ya mageuzi makubwa ya taasisi hiyo ya Uingereza yanayolenga kupunguza gharama huku ikikabiliana na changamoto za kifedha na ulipaji wa mkopo wa Pauni 197 milioni uliotolewa na Serikali ya Uingereza wakati wa janga la Uviko-19.

Dar es Salaam. Taasisi ya British Council imetangaza mpango wa kufunga ofisi yake nchini Tanzania ikiwa ni sehemu ya mpango mkubwa wa mageuzi unaolenga kupunguza gharama kutokana na shinikizo la kifedha.

Tanzania ni miongoni mwa nchi saba duniani ambazo zitapoteza uwepo wa ofisi za British Council, huku nchi nyingine za Afrika zilizoathirika zikiwa Botswana na Msumbiji.

Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na Gazeti la The Independent la Uingereza, hatua hiyo imechukuliwa baada ya taasisi hiyo kukabiliwa na changamoto za kifedha pamoja na jukumu la kurejesha mkopo wa Pauni 197 milioni  (Sh694.5 bilioni) uliotolewa na Serikali ya Uingereza wakati wa mlipuko wa virusi vya corona.

Nchi nyingine zitakazofungwa ofisi za British Council ni Chile, Peru, Croatia na Trinidad na Tobago.

British Council imesema pamoja na kufunga ofisi hizo, itaendelea kutekeleza programu zake za maendeleo na inatarajia kuendelea kupata kiwango kilekile cha ufadhili kutoka Serikali ya Uingereza kupitia mpango wa Msaada Rasmi wa Maendeleo (ODA).

Kwa miaka mingi, British Council imekuwa na nafasi muhimu katika kukuza uhusiano wa Uingereza na Tanzania kupitia programu za kujifunza lugha ya Kiingereza, ushirikiano wa elimu, sanaa, utamaduni na kubadilishana maarifa.

British Council ni taasisi ya Uingereza iliyoanzishwa mwaka 1934 kwa lengo la kukuza uhusiano wa kimataifa kupitia elimu, lugha, sanaa na utamaduni.