Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dereva bodaboda ashtakiwa kwa kujifanya mke wa makamu wa Rais

Watuhumiwa  Blaise Nabiswa na mwenzake Jacklyne Tokesi wakiwa katika Mahakama ya Mlimani nchini Kenya.

Muktasari:

  • Shtaka hilo liliwasilishwa kaitka Mahakama ya Mlimani nchini Kenya na Hakimu wa Mahakama ya Milimani Februari 18, 2023, Lukas Onyinga alieleza kuwa Blaise Nabiswa na mwenzake Jacklyne Tokesi wamewalaghai na kukusanya fedha kutoka kwa wananchi huku wakidai watawasajili katika Taasisi ya Mama Care Initiative Loan.

Kenya. Mwendesha bodaboda, Blaise Nabiswa ameshtakiwa kwa kufungua mtandao wa Facebook kwa lengo la kukusanya fedha na akijifanya mke wa Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua.

Shtaka hilo liliwasilishwa kaitka Mahakama ya Mlimani nchini Kenya na Hakimu wa Mahakama ya Milimani Februari 18, 2023, Lukas Onyinga alieleza kuwa Blaise Nabiswa na mwenzake Jacklyne Tokesi wamewalaghai na kukusanya fedha kutoka kwa wananchi huku wakidai watawasajili katika Taasisi ya Mama Care Initiative Loan.

Mahakama hiyo imeeleza kuwa watuhumiwa hao walikuwa wakiiwaeleza watu kuwa unadhaminiwa wa mikopo unatolewa na Dorcus Gachagua ambaye ni mkewe Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua.

Nabiswa na Tokesi walikana mashtaka matatu ikiwamo kumlaghai Esther Wanjiku Waweru.

Onyina aliamuru wawili hao waendelee kukaa katika magereza ya Viwandani na Lang’ata hadi watakapopata dhamana.

Awali, washtakiwa hao waliamriwa wafikishwe katika Mahakama ya City kisha kupangwa siku ya kusikilizwa  kesi inayowakabili.

Washtakiwa hao wanadaiwa walipokea fedha kutoka kwa watu mbalimbali wakidai kuwa watawadhamini kuwasomesha watoto wao sekondari na vyuo vikuu. Pia walidai watawalipia wagonjwa gharama za hospitali.