Iran yadai imerusha aina mpya ya roketi

Muktasari:

Taarifa za kurushwa kwa roketi hiyo zilitangazwa na shirika la habari la serikali jana Alhamisi na katika kuthibitisha walitoa video inayoonyesha urushaji wa roketi hiyo, ikisema kwamba hilo limetokea kwenye kituo cha anga za juu cha taifa hilo.

Tehran, Iran. Iran imesema imefanikiwa kurusha aina mpya ya roketi iliyoundwa kwa ajili ya kubeba satelaiti hadi kwenye anga la juu.

Taarifa za kurushwa kwa roketi hiyo zilitangazwa na shirika la habari la serikali jana Alhamisi na katika kuthibitisha walitoa video inayoonyesha urushaji wa roketi hiyo, ikisema kwamba hilo limetokea kwenye kituo cha anga za juu cha taifa hilo.

Chombo hicho kimesema kwamba roketi hiyo inaweza kubeba satelaiti yenye uzito wa hadi kilogramu 250 kwenye mzingo ulio umbali wa kilomita 500. Iran ilifanikiwa kurusha satelaiti yake ya kwanza mwaka 2009.

Nchi hiyo pia inadhamiria kupeleka satelaiti nyingi kwenye mzingo kwa ajili ya mawasiliano na sababu nyinginezo. Pia imeendelea na msimamo wake wa mpango wa makombora kwa kile inachodai kuwa ni kwa ajili ya kujinda.