Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Janga la moto lauwa watu zaidi ya 70 Afrika Kusini

Dar es Salaam. Moto uliozuka katika jengo la ghorofa tano katika jiji la Johannesburg, Afrika Kusini, umesababisha vifo vya zaidi ya watu 70, huku wengine wengi wakijeruhiwa.

Kwa mujibu wa mtandao wa DW, moto huo umetokea katika jengo lililopo katika eneo lenye shughuli nyingi za kibiashara la jiji hilo kubwa la Johannesburg.

DW imeripoti kuwa taarifa ya msemaji wa Kitengo cha Huduma za Dharura cha jiji hilo, Robert Mulaudzi, amesema moto huo pia umesababisha watu wengine takriban 52 kujeruhiwa.

Hata hivyo Mulaudzi amesema idadi ya vifo inaweza kuongezeka zaidi kwa kuwa jitihada ya kutafuta miili ya watu kutoka ghorofa moja kwenda nyingine inaendelea.

Katika taarifa yake ya ziada aliyoitoa kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X, kampuni ambayo awali iliyokuwa ikijulikana kama Twitter, msemaji huyo amesema watu kadhaa wameokolewa.

Hata hivyo pamoja na hiyo, msemaji huyo amenukuliwa na vyombo tofauti vya habari nchini Afrika Kusini, ambapo amesikika akisema jengo hilo lililowaka moto, lilikuwa limetelekezwa ila limefanywa makazi kwa wasio na malazi.

Lakini pia mbali ya vifo vilivyotokana na moto, vipo ambavyo vimetokana na baadhi ya watu ambao wanatajwa kufanya majaribio ya kuruka kutoka katika jengo hilo refu, kama njia ya kunusuru uhai wao wakati wa usiku, kipindi ambacho moto huo ulikuwa unaendelea kuwaka.

Msemaji Mulaudzi amenukuliwa akisema wanaendelea na shughuli za uokoaji katika jengo hilo.

 "Mara tu tunapomaliza, tunakabidhi eneo la tukio, kwa polisi kuendelea na kazi yao,alisema Mulaudz.

Eneo hilo la kati la Johannesburg limekuwa na majengo yaliyotelekezwa au kuanza kubomoka na mara nyingi yanatumiwa kama makazi na watu wenye shida ya malazi.

Mamlaka ya jiji huyataja aina hiyo ya majengo kama "majengo yaliyotekwa nyara," duru zinaeleza jengo hilo lilikuwa na wakazi takribani watu 200.

Shuhuda mmoja ambae anaishi karibu na jengo hilo amekiambia kituo kimoja cha televisheni nchini Afrika Kusini kuwa wakati moto ulipoanza, alisikia sauti ya vilio vya watu vya kuomba msaada, wakisema "wanakufa".

Hadi wakati huu chanzo rasmi cha moto huo, bado hakijajulikana na maafisa wanaendelea na uchunguzi wao.

Lakini Afisa mmoja wa Serikali za mitaa katika eneo hilo, Mgcini Tshwaku, amesema inaonekana kama kuna mkazi mmoja aliwasha moto kwa lengo la kupasha joto makazi yake ili kujikinga na hali ya baridi kali.