Jeshi Guinea lachukua nchi, hatima ya Rais shakani
Muktasari:
- Jeshi nchini Guinea limesema limeiweka nchi hiyo chini ya utawala wake, huku hatima ya Rais Alpha Condé ikiwa haijajulikana baada ya video ambayo haijathibitishwa ikimuonyesha yumo mikononi mwa wanajeshi waliodai kufanya mapinduzi.
Jeshi nchini Guinea limesema limeiweka nchi hiyo chini ya utawala wake, huku hatima ya Rais Alpha Condé ikiwa haijajulikana baada ya video ambayo haijathibitishwa ikimuonyesha yumo mikononi mwa wanajeshi waliodai kufanya mapinduzi.
Video hiyo imesambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikimwonesha Rais Conde akishikiliwa na wanajeshi kisha akasukumwa kwenye gari na kupelekwa mbali.
Kiongozi wa jeshi hilo, Mamady Doumbouya wa jeshi amesema katika video iliyorekodiwa kwenye mji mkuu wa Conakry kwa njia zote za usafiri pamoja na mipaka ya nchi imefungwa kwa muda, huku akiwaomba wananchi wabaki majumbani wakisubiri maelekezo zaidi juu ya mwelekeo wa serikali.
Amesema moja ya sababu ya kufanya hivyo ni kutokana na Rais Conde kushindwa kutekeleza ahadi zake kwa watu wa Guinea.