Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiongozi wa upinzani Ghana ashinda urais

Rais mteule wa Ghana, John Mahama

Accra. Rais wa zamani wa Ghana, John Mahama ambaye pia ndiye kiongozi mkuu wa upinzani nchini humo, ameshinda tena urais katika uchaguzi mkuu uliofanyika jana Jumamosi, Desemba 7, 2024.

Mahama aliwahi kuwa Rais wa nchi hiyo katika muhula wa mwaka 2012 hadi 2017.

Kiongozi huyo ambaye pia alikiwakilisha chama cha National Democratic Congress (NDC), amemshinda Makamu wa Rais wa nchi hiyo, Mahamudu Bawumia aliyekuwa akikiwakilisha chama tawala cha New Patriotic Party (NPP).

Kabla ya tangazo hilo rasmi, Bawumia aliwaambia waandishi wa habari kwamba anaheshimu uamuzi wa Waghana kupiga kura kwa ajili ya mabadiliko. "Nimempigia simu Mheshimiwa John Mahama kumpongeza kama Rais mteule wa Jamhuri ya Ghana.”


Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi