Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Korea Kaskazini yaonyesha Makombora yake ya Masafa marefu

Makombora ya masafa marefu ya Korea Kaskazini yakipita mbele ya kiongozi Kim Jong Un wakati wa gwaride la kijeshi la Jumatano usiku huko Pyongyang.

Muktasari:

  • Korea Kaskazini imeonyesha takriban makombora kumi na mawili ya hali ya juu ya masafa marefu katika gwaride la kijeshi la usiku wa Jumatano, katika onyesho kubwa zaidi la kile ambacho vyombo vya habari vya serikali yake vilikielezea kuwa "uwezo wa mashambulizi ya nyuklia".

Dar es Salaam. Korea Kaskazini imeonyesha makombora yake ya masafa marefu (ICBMs) onyesho ambalo linatajwa kuwa kubwa zaidi kuwahi kutokea.

Takribani dazeni za ICBM za masafa marefu zilioneshwa kwenye gwaride la kijeshi la lililofanyika siku ya Jumatano.

Kwa mujibu wa CNN imeripoti kuwa Makombora yalirushwa kupitia uwanja wa Pyongyang huku kiongozi Kim Jong Un akiwa ameandamana na mkewe na msichana mdogo anayeaminika kuwa binti yake.

Tukio hilo lilikuwa ni kumbukumbu ya kuanzishwa kwa jeshi la Korea Kaskazini, na linakuja miezi miwili baada ya Kim kutoa wito wa "ongezeko kubwa" la silaha za nyuklia za nchi yake kujibu kile anachodai ni vitisho kutoka Korea Kusini na Marekani.

Mwaka jana ilishuhudia Korea Kaskazini ikifanyia majaribio makombora mengi zaidi kuliko wakati wowote katika historia yake, likiwemo kombora la balestiki la intercontinental (ICBM) ambalo kwa nadharia linaweza kushambulia Marekani.

Gwaride hilo lilifuatia karamu ya kifahari usiku wa mapema ambapo Kim alimweka msichana anayeaminika kuwa binti yake Ju Ae, ikiwa ni ishara kwamba msichana huyo anaweza kuandaliwa kama mrithi wake.