Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mafuriko yaua sita Afrika Kusini

Moja kati ya maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko Afrika Kusini.

Muktasari:

  • Watu wengine 10 hawajulikani walipo kutokana na mvua kubwa kunyesha na kusababisha mafuriko yaliyosababisha maafa hayo nchini humo.

Afrika Kusini. Watu sita wamefariki dunia, huku wengine 10 wakiwa hawajulikani walipo baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha mafuriko yaliyoleta maafa hayo nchini humo, polisi wamesema.

Vikosi vya uokoaji vimeanza kutafuta miili leo Jumanne Desemba 26, 2023 baada ya mvua kubwa kunyesha katika mji wa Ladysmith, usiku wa kuamkia Jumapili na kusomba magari kutoka barabara kuu na kusababisha watu kushindwa kutoka nje, mamlaka ya mkoa wa KwaZulu Natal imesema.

"Kwa sasa tuna watu sita waliothibitishwa kufariki dunia na bado watu 10 hawajulikani walipo. Tunaendelea na juhudi za kuwatafuta," msemaji wa polisi ameiambia AFP.

Ameongeza, “Miili mitatu ilipatikana katika basi dogo lililokuwa limebeba abiria tisa. Wengine sita bado hawajulikani walipo,” amesema msemaji huyo.

Mwili mmoja umepatikana katika nyumba iliyoharibiwa, huku watu wengine wawili ambao pia walikuwa ndani wakiwa bado hawajulikani walipo.

Takriban watu wengine wawili wamepoteza maisha baada ya kukwama kwenye magari yao na mafuriko katika mto Bellspruit.

Hali ya mvua na upepo mkali inatarajiwa kuendelea kuyakumba maeneo yaliyoko ufukweni mwa bahari nchini humo.