Majaji waghairi kumshtaki mtuhumiwa aliyefikisha miaka 90 mauaji ya kimbari

Felicien Kabuga

Muktasari:

Mahakama ya uhalifu wa kivita ya Umoja wa Mataifa, imesema mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda yaliyofanyika mwaka 1994 mwenye umri wa miaka 90 kuwa hana tena uwezo wa kushiriki kesi kikamilifu.



The Hague. Mahakama ya uhalifu wa kivita ya Umoja wa Mataifa, imesema mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda yaliyofanyika mwaka 1994 mwenye umri wa miaka 90 kuwa hana tena uwezo wa kushiriki kesi kikamilifu.

“Felicien Kabuga Mtuhumiwa wa mauaji ya halaiki Rwanda hastahili tena kushitakiwa,” wamesema majaji wa mahakama hiyo.

Kabuga amekuwa akikwepa kukamatwa kwa miaka kadhaa lakini Mei, 2020 alikamatwa nyumbani kwake Paris na baadaye kufikishwa kwenye Mahakama ya Umoja wa mataifa ya uhalifu wa kivita ambapo aliingia katika ombi la kutokuwa na hatia.

Kesi ya Kabuga imeanza kusikilizwa Septemba, 2022 lakini aligoma kufika mahakamani mwanzoni mwa kesi yake, Kabuga amekua akisikiliza kesi kupitia video katika viunga vya mahakama hiyo.

Mfanyabiashara huyo wa zamani nchini Rwanda, ambaye alipata utajiri kupitia biashara ya kilimo cha chai, ni mmoja wa watuhumiwa wa mwisho waliotafutwa na mahakama hiyo inayoendesha mashitaka ya uhalifu uliofanyika katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.