Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mlipuko wa gesi waua 13 kiwandani Qatar

Muktasari:

  • Waziri wa Nishati wa Taifa hilo Saad al-Kaabi amesema kuwa idadi kubwa ya waliopoteza maisha ni raia wa Pakistani na wahindi waliokuwa wakifanya kazi katika kiwanda hicho na wengine ni wale waliokuwa karibu mazingira ya kiwanda hicho.

Doha. Watu 13 wameripotiwa kufariki dunia huku 66 wakijeruhiwa kutokana na mlipuko wa gesi uliotokea katika kiwanda cha kusindika gesi nchini Qatar.

Tukio hilo limetokea siku mbili baada ya kiwanda hicho kuanza tena shughuli za uzalishaji, usindikaji na usambazaji wa Gesi baada ya kufungwa kwa muda wa miezi sita ili kupisha matengenezo yaliokamilika siku mbili zilizopita na kupelkea kufunguliwa tena kwa kiwanda hicho.

Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Nishati wa Taifa hilo, Saad al-Kaabi imeleza kuwa mlipuko huo umetokea wakati wa kuanza upya kwa shughuli za usindikaji  katika kituo Barzan ambacho pia hufanya kazi ya usambazaji wa gesi ndani ya Taifa hilo.

“Watu kumi na watatu waliuawa na makumi kadhaa kujeruhiwa katika mlipuko kwenye kituo cha kusindika gesi ndani ya kiwanda kikubwa cha Ras Laffan katika moja ya ajali mbaya zaidi kwenye sekta hii ndani kipindi cha miongo miwili,” amesema Kaabi.

Waziri huyo amesema kuwa, idadi kubwa ya waliopoteza maisha ni raia wa Pakistani na wahindi waliokuwa wakifanya kazi katika kiwanda hicho huku wengine ni wale waliokuwa karibu mazingira ya kiwanda hicho.

Ameongeza kuwa baada ya tukio hilo mamlaka inahusika na sekta hiyo Qatar Energy imeanza uchunguzi kamili kuhusu chanzo cha ajali hiyo, ambayo kiongozi huyo  amesisitiza kuwa  haikuwa hujuma au uadui kama inadhaniwa na baadhi ya watu.

Katika hatua nyingine mamlaka ya usimamizi wa nishati ya gesi nchini humo QATAR Energy LNG imesisitiza kufungwa kwa vituo kadhaa vya uzalishaji wa mafuta na gesi katika kipindi hiki ambacho mgogoro baina ya Marekani na Iran unaendelea katika eneo la mashariki ya Kati.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Ahmed Al -Mohamed imesema kuwa hatua inalenga kuimarisha ulinzi na kuondoa hatari zisizo za lazima zinazoweza kuepukika ikiwa vikosi vya Iran vitafanya mashambulizi katia maeneo hayo au maeneo ya Jirani.

Kutokana na Taifa hilo kuwa na kambi kubwa ya kijeshi ya Marekani, jambo linaloilazimu Iran kulitazama Taifa hilo kwa jicho la tatu kutokana na uwezekano wa Marekani kulitumia kama ngome ya kufanikisha mashambulizi yake kwa Taifa la Iran.

Kama ilivyofanywa kipindi kilichopita na kuilazimu Iran kujibu kwa kushambulia eneo  Ras Laffan ambalo lilikuwa na uwezo wa kuzalisha tani  milioni 77 za gesi kila mwaka kabla ya kuharibiwa kwa miundombinu ya  treni mbili, na kupunguza asilimia 17 ya uzalishaji.


Imeandikwa na Elidaima Mangela kwa msaada wa mashirika ya Habari