Polisi nchini Pakistan wadaiwa kuwazuia wanahabari kupata taarifa

Jeshi la Polisi nchini Pakistan limewashinda waandishi wa habari katika ombi lao la kutaka kusajiliwa kwa ripoti tofauti ya kwanza ya habari (FIR) dhidi ya polisi kwa kuwashikilia waandishi wa habari nje ya Mahakama Kuu ya Islamabad Februari 28, mwaka huu.

Mahakama ya wilaya katika mji mkuu wa nchi hiyo, Jumamosi iliyopita iliamuru kurekodi taarifa za vyombo vya habari katika kesi ya ugaidi kuhusu tukio hilo, Geo News iliripoti.

Polisi waliwazuia waandishi wa habari wakati mwenyekiti wa Pakistan Tehreek-e-Insaf (PTI), Imran Khan alipofikishwa mbele ya mahakama ya Islamabad katika kesi nyingi zinazomkabili zikiwemo za jaribio la mauaji, ufadhili uliopigwa marufuku.

Geo News iliripoti kwamba kiongozi huyo wa PTI alipowasili katika mahakamani, wafanyikazi wengi wa PTI waliingia ndani ya jengo hilo kwa kuvunja mlango.

 Mipangilio ya usalama katika mahakama hiyo ilishindwa kufanya kazi huku wafanyakazi hao wakiondoa vizuizi vyote.

Saqib Bashir ambaye ni mwandishi wa habari aliitaka mahakama kusajili kesi ya jinai dhidi ya polisi chini ya vifungu husika akidai kuwa aliwasilisha maombi polisi lakini hayakuzaa matunda.

Februari 28, Polisi wa Jimbo kuu la Islamabad (ICT) walisajili kesi ya ugaidi kwa madai ya uharibifu, ghasia na hujuma katika mahakama ya mji mkuu wakati mwenyekiti wa PTI akifikishwa mbele ya mahakama tofauti kuhusiana na kesi nyingi zilizowasilishwa dhidi yake.

Wakati wa shauri hilo, wakili wa mwanahabari huyo alidai kuwa mteja wake hana wasiwasi wowote na waandamanaji wa chama cha siasa au vitendo vinavyofanywa na wao na tukio lililofanyika kwake linaweza kutofautishwa.

Katika hukumu yake Jaji Tahir Abbas Sipra aliamuru kurekodi taarifa za mlalamishi na waandishi wengine wa habari katika kesi ya ugaidi.