Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Rais Mnangagwa ashinda kwa 50.8%

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa matangazo yaliyotolewa na Tume ya Uchaguzi Zimbabwe (ZEC) Ijumaa asubuhi, Mnangagwa, wa chama tawala cha Zanu PF ameshinda kwa kura 2,460,463 sawa na asilimia 50.8 huku mshindani wake mkuu Nelson Chamisa wa muungano wa upinzani wa Movement for Democratic Change (MDC) akijikusanyia kura 2,147,437 sawa na asilimia 44.3.

Harare, Zimbabwe. Rais Emmerson Mnangagwa amewashukuru Wazimbabwe kwa kumpa kura za ushindi katika uchaguzi uliofanyika kwa amani na utulivu lakini zikatokea vurugu katika maandamano ya kupinga matokeo.
“Nawashukuru Wazimbabwe! Nimefurahishwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe. Ingawa tuligawanyika wakati wa uchaguzi mkuu, tumeunganika katika ndoto zetu. Huu ni mwanzo mpya. Hebu tushikane mikono, katika amani, umoja na upendo, tujenge Zimbabwe mpya kwa wote!” alisema kwa ujumbe wa Twitter.
Kwa mujibu wa matangazo yaliyotolewa na Tume ya Uchaguzi Zimbabwe (ZEC) Ijumaa asubuhi, Mnangagwa, wa chama tawala cha Zanu PF ameshinda kwa kura 2,460,463 sawa na asilimia 50.8 huku mshindani wake mkuu Nelson Chamisa wa muungano wa upinzani wa Movement for Democratic Change (MDC) akijikusanyia kura 2,147,437 sawa na asilimia 44.3.
Ili mgombea urais atangazwe mshindi alikuwa anapaswa kupata kura asilimia 50 jumlisha moja.
Mnangagwa, aliyewahi kuwa makamu wa rais na akifahamika kwa jina la “mamba” kwa sababu ya werevu wake kisiasa, amekuwa madarakani tangu Novemba 2017 baada ya kujiuzulu kwa mtangulizi wake Robert Mugabe chini ya shinikizo la jeshi.
Mara baada ya matokeo hayo kutangazwa, Mnangagwa alituma ujumbe wake kwa Twitter akiwashukuru Wazimbabwe na akawapongeza kwa "mwanzo mpya".
Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 75 ameahidi kurejesha uwekezaji wa kigeni pamoja na kutengeneza nafasi nyingi za kazi.
Msemaji wa Zanu PF, Paul Mangwana alisema chama tawala “kimefurahishwa mno na matokeo".
"Tumefurahishwa kwamba rais wetu ameshinda kwa sababu hii ina maana sasa tunaweza kufanya mageuzi yaliyoahidiwa kwa wananchi,” Mangwana aliliambia shirika la Al Jazeera.
Hata kabla ya matokeo ya urais kutangazwa, chama cha MDC kiliishutumu serikali kwa kuiba matokeo ya uchaguzi huo wa kwanza bila jina la Mugabe kuwemo kwenye karatasi za kupigia kura.
"Tumeshinda uchaguzi huu na Mnangagwa anafahamu. Wafuasi wetu wanaombwa wabaki watulivu huku wakitarajia kufanya sherehe za nguvu," alisema Chamisa mapema Alhamisi baada ya kuwatembelea majeruhi katika hospitali ya Parirenyatwa mjini Harare.
Watu watatu waliuawa na askari waliofyatua risasi kuzima maandamano ya wafuasi wa MDC waliokosa uvumilivu kutokana na ZEC kuchelewa kutangaza matokeo ya urais.